Mwanahabari maarufu wa Kenya Betty Mutei Kyallo ameendelea kujigamba kuhusu uhusiano wake mpya na kijana Charlie Jones. 

Siku ya Jumapili, mtangazaji huyo wa TV47 alikiri kwamba hatimaye anahisi kupendwa baada ya kupitia dhiki nyingi hapo awali.

Betty alidokeza kwamba aliteseka sana katika mahusiano ya zamani na akasema kwamba hangependa hata Charlie ajue kuhusu yale ambayo amepitia.

“Mtoto wa kike kapendwa, hatimaye. Hata sitaki ajue maneno nimepitia, ilikuwa mbaya bruh. Lakini sasa uko hapa,” Betty Kyallo alisema.

 

Mwanahabari huyo mrembo aliendelea kuonyesha matukio kadhaa mazuri aliyokuwa nayo na mpenzi wake huyo  wa miaka 26. 

Uhusiano wa Betty na Charlie hatimaye ulikuja kujulikana wazi miezi michache iliyopita baada ya mtangazaji huyo wa TV kujaribu kumficha mpenzi wake kwa muda.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hatimaye Betty Kyallo alifichua sura ya mpenzi wake mwezi Juni huku akimsifia katika ujumbe mzuri wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa.

 

Ufichuzi huo ulikuja saa chache baada ya mwanahabari huyu kuwajibu wakosoaji wake kwa tamko la uhakika la furaha yake, akisema kwamba yeye ni "mke mwenye furaha anayefurahia maisha ya furaha."

 

Betty na mpenzi wake walitumia siku ya kimapenzi huko Ngong Hills, ambapo alishiriki sala maalum na kumtakia tamu alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

"Heri ya kuzaliwa, mpenzi. Vicheko zaidi, kukumbatiana zaidi, watoto zaidi, sisi zaidi. Hii ndio. Naomba mtu wangu ashinde kila wakati. Amekuwa akishinda, lakini nataka ashinde mengi zaidi. Kwa Mungu, mke mwenye furaha, maisha ya furaha. Type shii,” aliandika.

Wawili hao hata hivyo wamekabiliwa na ukosoaji mwingi mtandaoni kuhusu tofauti zao za umri huku Betty Kyallo akiwa na umri wa miaka kadhaa kuliko mpenzi wake.