Jengo la orofa nyingi lenye nyumba za makazi na biashara kadhaa limeripotiwa kuporomoka katika eneo la Kahawa West, Nairobi  siku ya Jumapili adhuhuri.

Familia kadhaa zinahofiwa kukwama ndani ya jengo hilo ambalo kuanguka kwake kulirekodiwa katika video zinazovuma kwenye mitandao ya kijamii.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kuwa timu imetumwa kusaidia shughuli ya uokoaji.

"Timu ya mashirika mengi ya kukabiliana na matukio kwa sasa inajibu kufuatia kuporomoka kwa jengo katika eneo la Kahawa Magharibi, Kaunti ya Nairobi, ambapo watu wanahofiwa kunaswa." Msalaba Mwekundu alisema katika taarifa.

Taarifa zaidi zitafuata punde tutakapozipata...