Rapa mkongwe wa Kenya Paul Julius Nunda almaarufu Jua Cali anaonekana kuendelea kupata nafuu vizuri baada
ya kulazwa hospitalini kutokana na maradhi.
Siku ya Ijumaa, mwimbaji huyo wa nyimbo za genge alionekana
kwenye posti za mitandao ya kijamii akiwa na familia na marafiki waliomtembelea
hospitalini.
Mwimbaji huyo alichapisha picha za watu mashuhuri kama vile
mwanamuziki Wyre, Ala C na mwanamitindo Bashir miongoni mwa wengine
waliomtembelea hospitalini. Pia anaonekana akifurahia muda na watoto wake
waliokwenda kumtembelea.
"Shukran sana @alacgenge @wyredalovechild kwa kucome
thru, shukran," Jua Cali alisema katika moja ya machapisho yake.
Katika post nyingine, alionekana akiwa amewashika binti zake
ambao pia walikuwa wamemtembelea wodini.
"Watoto wangu walinijia ili kuniweka sawa,"
aliandika.
Siku ya Ijumaa, wasimamizi wa Jua Cali kupitia kwa meneja wake
Collins Odindo walisema mwimbaji huyo hatacheza katika shoo zijazo kulingana na
maagizo ya madaktari.
"Tunasikitika kukujulisha kuwa Jua Cali kwa sasa yuko
hospitali chini ya uangalizi." Walisema.
Alisema madaktari wa mwimbaji huyo wamemshauri kukaa kwenye
mapumziko ya kitanda na chini ya uangalizi kwa siku mbili hadi tatu zijazo.
Akiongeza, "Tumesikitishwa sana na mabadiliko haya ya
matukio haswa kama inakuja kabla ya maonyesho yake ambayo yanatarajiwa wikendi
hii."
"Mawazo yetu yako kwa Jua Cali na tunamtakia ahueni ya
haraka., Pia tunatoa usaidizi wetu kwa familia, marafiki na mashabiki wakati
huu."
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!