Mfanyibiashara maarufu wa vipodozi Being Amira amepuuza nafasi yoyote ya yeye kurudiana na aliyekuwa mume wake Jimal Marlow Rohosafi.
Amira alitangaza hayo baada ya mtumizi wa mtandao wa tiktok kumuita mfanyabiashara Jimal Rohosafi amchukue.
Mama huyo wa wavulana wawili alikuwa amechapisha video nzuri inayoonyesha sura yake mpya ya mwili baada ya kuufanyia kazi kwa muda.
"Jimal kujia Mali yako," shabiki alitoa maoni chini ya chapisho la Amira.
Katika majibu yake, Amira alibainisha kwamba baba wa watoto wake wawili si wa aina yake tena.
"Yeye sio aina yangu tena, lo," alijibu.
Haya yanajiri takriban miaka mitatu baada ya Amira kutoa talaka kwa mfanyabiashara huyo maarufu wa Nairobi.
Jimal na Amira walitalikiana rasmi mwaka wa 2022 baada ya utengano uliotangazwa sana.
Tofauti zao zilitokea baada ya Jimal kuoa sosholaiti Amber Ray kama mke wake wa pili, ambaye hakuwa akielewana na Amira.
Mama huyo wa watoto wawili alimkataa mke mwenza wake Amber Ray na mapigano na ugomvi usioisha ulishamiri kwenye ndoa yao na mfanyabiashara huyo Msomali.
Wakati wa kuachana kwao, Amira alienda moja kwa moja kutoa maelezo kuhusu kilichojiri kati ya alipoamua kuolewa na Jamal na mfanyibiashara huyo alipoanza kumlaghai na Amber Ray.
Mfanyabiashara huyo alidai kuwa wakati mmoja, alipoteza ujauzito wake baada ya mumewe kumpiga.
Jamal alikanusha madai hayo.
Kupitia screenshotm, Amira pia alidai kuwa Jamal hakuwa akiwaandalia watoto wao mahitaji.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!