Mwanasiasa na wakili aliyezingirwa na utata mwingi Karen Njeri Nyamu anaonekana kufurahishwa na kijana mmoja aliyetunga wimbo akikiri kumpenda.
Kijana huyo alibadilisha maneno ya wimbo ‘Binti Kiziwi’ wa Marlaw na kuweka maneno ya kueleza mapenzi mazito kwa seneta huyo wa kuteuliwa.
Huku akitoa maoni kuhusu wimbo huo, Bi Nyamu aliomba kusaidiwa kumfikia kijana huyo akidokeza kuwa yuko tayari kumpa moyo wake.
“Nani ako na namba ya huyu nataka kurisk mapenzi tena,” Karen Nyamu alisema chini ya video ya wimbo huo ambayo alichapisha kwenye Facebook.
Katika wimbo huo mfupi, kijana huyo alikiri jinsi anavyovutiwa na seneta huyo wa kuteuliwa na kudai kuwa yuko tayari kuwa kwenye mahusiano naye.
““Nakuja na njia zote madam si unanimaliza. Call me daddy, sugar daddy kwa lemon naadd sugar. Nakuanga captive kwa mapenzi umenifunga. Unaweza niita Mr County na kwangu we ndo senator.
Napenda vile uko shida zako siangalii na napenda unavyonipa kwa wengine sitamani. Nafeel different vybe whenever nikiwa nawe tukiwa wawili siongei, mapenzi nataka nipewe.
Your smile na figure ndo inafanya nataka more. Nataka nikuje kwenyu tukutane Karenzo, coz in my mind ur business. Tukiongea furthermore tuende park, tukachill na mabreeze mambo mnoo,” aliimba kijana huyo.
Kwa muda sasa, hali ya uhusiano wa seneta Karen Nyamu imekuwa ya kitendawili hasa tangu alipoacha kutangaza mambo yake ya kibinafsi mapema mwaka huu.
Kwa muda sasa, hajatangaza wazi wazi mapenzi yake na mzazi mwenzake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, kama alivyokuwa akifanya hapo awali.
Hili limezua wasiwasi miongoni mwa wafuasi wake, wengine wakiamini kuwa uhusiano wao wa miaka mingi unaweza kuwa umeisha.
Bi Nyamu na baba huyo wa watoto wake wawili pia hawajaonekana pamoja kwa muda mrefu sasa, kama walivyokuwa wakionekana hapo awali.
Mapenzi ya hadharani kati ya wazazi wawili hao yalionekana kupungua kuanzia takriban miezi mitatu iliyopita wakati Samidoh alipofunga safari hadi Marekani kumtembelea mke wake wa kwanza Edday Nderitu na watoto wao watatu.
Wawili hao walionekana kuwa na wakati mzuri huko na familia yao.
Katika picha na video ambazo zilirekodiwa nchini Marekani mwezi Juni, wazazi hao wawili walionekana kuwa na furaha pamoja na kushikana kama watu wanaopendana.
Hii ilibua tena maswali tata kuhusu hali halisi ya ndoa ya wawili hao ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya muongo mmoja hadi mwaka jana wakati ambapo Edday pamoja na watoto wao watatu walihamia Marekani na kumuacha Samidoh nchini Kenya.
Bi Edday Nderitu kwa sasa anaishi Marekani pamoja na watoto wao watatu. Aliondoka nchini mapema mwaka jana na anaonekana tayari kutulia huko vizuri huku watoto wakiwa wameanza shule huko.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!