Wanawake na vijana wanahimizwa kuongeza juhudi katika kuzuia ghasia zinazohusiana na uchaguzi, huku Kenya ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Wadau wa amani, maafisa wa Kaunti ya Kilifi, na mashirika ya kiraia wanasema kuwa ushiriki wao kikamilifu ni muhimu sana katika kutatua migogoro ya kijamii na kudumisha usalama. Mkurugenzi wa Masuala ya Jinsia na Vijana katika Kaunti ya Kilifi, Mwangome Shumaa, anasema kuwa kuwawezesha wanawake kuwa mstari wa mbele katika kukuza amani, kusuluhisha migogoro, na kushiriki katika uongozi ni hatua muhimu ya kuzuia ghasia.
MWANGOME SHUMAA – WOMEN