Wahitimu wa NYS watapangiwa majukumu ya kulinda taasisi za serikali iwapo wabunge wataidhinisha hoja iliyowasilishwa na Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Kilifi, Gertrude Mbeyu. Hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni inaangazia umuhimu wa kuwa na mkakati wenye uwiano unaochochea ajira kwa vijana kupitia ushirikishwaji uliopangwa wa wahitimu wa NYS, huku pia ukilinda fursa za kampuni binafsi za ulinzi kuendelea na shughuli zao na kushirikiana na taasisi za serikali.