Rais William Ruto amesema upinzani unachochea hasira, ukabila na wivu. Akizungumza huko West Pokot, Ruto aliwashutumu viongozi wa upinzani kwa kukosa ajenda ya wazi ya maendeleo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Ruto alilinganisha mipango ya serikali yake na ile ya upinzani, akielezea tofauti hiyo kuwa kubwa kama ile ya mchana na usiku. Aliahidi kuendelea kuukosoa upinzani, akisema Wakenya wanastahili viongozi wenye mtazamo wa maendeleo na waliojitolea kwa ustawi wa taifa.

WILLIAM RUTO –ANGER