Kuna hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu usimamizi wa mtihani wa KCSE ya mwaka 2026, huku chama cha walimu KUPPET kikisisitiza tishio lake la kususia zoezi hilo kutokana na malipo duni. Ratiba ya Baraza la Mitihani nchini (KNEC) inaonyesha kuwa rehearsal za mtihani huo zitafanyika Ijumaa, zikifuatiwa na mitihani ya maneno na vitendo kuanzia tarehe 19 Oktoba. Ratiba hii itaingiliana na ile ya KPSEA na KJSEA, ambayo rehearsal zake zimepangwa kufanyika Ijumaa, tarehe 23 Oktoba, kabla ya kuanza kwa mitihani ya maandishi siku ya Jumatatu, tarehe 26.