Kamati ya Bunge ya Haki na Masuala ya Kisheria imeunga mkono wito wa kufutwa kwa adhabu ya lazima ya kifo nchini Kenya. Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwengi Mutuse, anasema Bunge linaangazia kuweka mfumo wa kisheria wa kuondoa adhabu hiyo. Akizungumza katika mkutano na Tume ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo, Mbunge huyo wa Kibwezi Magharibi alisema Kenya imepiga hatua kubwa, akibaini kuwa mara ya mwisho kutekelezwa hukumu ya kifo ilikuwa mwaka wa 1987.