Mamlaka ya EPRA leo itatangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kwa mwezi mmoja ujao. Katika mapitio ya mwezi uliopita, mamlaka hiyo ilidumisha bei za  'Super petrol, dizeli na mafuta ya taa. Hatua hii inakuja wakati serikali ikijaribu kuongeza muda wa kutekeleza viwango vilivyopunguzwa vya Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT) wa asilimia 8 kwa bidhaa za mafuta kwa siku nyingine 90, ili kuwapunguzia Wakenya mzigo wa gharama kubwa za mafuta.