Fulham wamevunja ukimya dakika ya 55 kupitia Raúl Jiménez, aliyepachika mpira wavuni kwa shuti la hakika kufuatia pasi murwa. Goli hilo linawaweka wenyeji mbele ya Chelsea 1–0, huku hali ugani Craven Cottage ikizidi kupamba moto.

22' Marc Cucurella alishwa kadi nyekundu. The Blues wanabaki wachezaji kumi ugani.

1' Muamizi anapuliza kipenga chake kuashiria mwanzo wa mechi... Mchuano wa Chelsea dhidi ya Fulham ugani Craven Cottage unakuja wakati nyeti kwa The Blues, ambao wanatafuta mwelekeo mpya baada ya kuondoka kwa kocha Enzo Maresca.

Chelsea wanashika nafasi ya tano kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa wamezoa jumla ya alama 31, lakini pengo la pointi 17 dhidi ya viongozi Arsenal linaakisi changamoto kubwa iliyopo mbele yao katika mbio za ubingwa. Je, watatamba chini ya Calum McFarlane? Tony Mballa