Duale akiongoza kikao cha kamati ya afya

Waziri wa Afya Aden Duale mnamo tarehe 23 Aprili, 2025 alikuwa na mkutano na viongozi pamoja  na washikadau wa afya.

 Ni mkutano ambao uliongozwa na waziri Duale akiwa pamoja na mkuu wa maafisa wa usafi wa  matabibu  Profesa Samweli Kang'ethe kujadili masuala  muhimu ya afya  pamoja  na usalama chini ya mfumo wa afya  kwa wote UHC.

 Akirejelea kifungu 33(2) cha  mwaka wa 2023  bima  ya afya  kwa wote waziri aliweza  kusisitiza  kuhusu ombi la kamati la  kuweza kudumisha madili ,ushahidi uliopo na  uwazi katika  kupatiana vibali vya kuhudumu pamoja  na kufanya ukaguzi maalim wa vifaa vya  matumizi katika hosipitali   mbalimbali.

Katika kutoa  muongozo maalum Duale aliweza kuwelezea  akisema kuwa kibali kisipewe kwa  afisa yeyote  wa  afya  ambaye amesomea  katika kituo  cha afya ambacho hakijaidhinishwa rasmi, Kukaguliwa, kupigwa msasa na kamati maalum ya  afya kutoka kwa  wizara ya afya.

Kwa kuweza kuzingatia  hayo tutakuwa  tunalinda viwango vyetu vya  afya  pamoja na mifumo yetu ya matibabu katika  ngazi zote  za hospitali za afya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwa kuhakikisha uwajibikaji waziri aliweza  kuamuru kamati iweze kuanzisha uchunguzi katika  mifumo yote  ya afya na iweze  kutuma  ripoti  ya hospitali  zote  ambazo zimesajiliwa  na wizara  ya afya pia aliweza  kusisitiza habari  zote  na rekodi zote  za afya ziweze kuhifadhiwa  kidijitali.

 Aliweza  kuamuru kwa kusema kuwa habari zote  za  hospitali ziweze  kuwekwa katika mfumo wa afya wa kidijitali wa serikali  ili kuweza  kuepukika  na kupotea kwa rekodi pamoja  na kusaidia kuweka viwango vyema vya ukaguzi.

Vilevile waziri aliwahakikishia wanajopo  kuwa wizara ilikuwa radhi kujitolea na  kushirikiana na washikadau pamoja  na kuendeleza kampeni ya bima  ya matibabu ya Taifa care pamoja  na mfumo wa maendelezo wa  ajenda  ya mabadiliko ya uchumi alimaarufu BETA.

Waliokuwepo katika  mkutano huo ni Katibu mkuu katika wizara ya Afya Mary Muthoni,mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya Daktari Patrick Amoth  na kaimu mshikilizi wa wizara ya uchumi wa digitali Bwana Anthony Lenaiyara.