watu wanajikinga mvua

Wizara ya hali ya anga imetangaza maeneo mbalimbali ya  taifa yatakayoshuhudia mabadiliko  ya hali ya anga.

Kulingana na idara hiyo, Nairobi itashuhudia mvua na hatimaye viwango vichache  vya jua  mchana huku kiwango cha juu cha  joto kikipanda  kwa nyusi 27 na kushuka kwa  asilimia 16.

Jijini Mombasa kutashuhudiwa viwango vya kadri vya  jua mchana kutwa  huku kiwango cha joto kikipanda kwa nyusi 33 na kupungua kwa nyusi 25 mtawalia.

Jijini Eldoret kutashuhudiwa vivango vya kadri  vya jua mchana kutwa huku kukishuhudiwa kiwango cha juu cha joto kwa nyusi 24 huku kiwango cha chini zaidi kikiwa ni nyusi 14.

Kulingana na ripoti ya  utabiri wa hali ya anga Maeneo ya Nakuru yatashuhudia viwango vya kadri vya jua mchana huku kiwango cha joto cha juu kikiwa ni 26 huku cha chini kikiwa 15.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maeneo ya Nyeri yatashuhudia viwango vya mvua pamoja na jua mchana huku kiwango cha joto cha juu kikiwa ni 26 na cha chini kikiwa ni 15.

Maeneo ya Marsabit kulingana na ripoti ya  utabiri wa hali ya anga kutashuhudiwa viwango vya mvua pamoja  na joto la kadri  huku kiwango  cha juu sana cha joto kikiwa 25 na cha chini 15

Katika kaunti ya Kakamega kutashuhudiwa viwango vya jua la wastani mchana huku viwango vya joto vikiwa  ni 28 kwa kiwango kikuu na 18 kiwango cha chini mtawalia.

Idara hiyo ya utabiri wa hali ya anga iliwataahadharisha wakenya wote kuwa makini wanaposafiri na kuwashauri kuhakikisha kuwa wanabeba na  kuvalia nguo nzito wanaposafiri ili kuepuka kupatwa na maradhi ya ghafla.

Vilevile utabiri huo uliwarahihishishia  na kuhakikisha kuwa wale  wote waliokuwa na ratiba ya kusafiri wanajipnga kwa uzuri na  kwa wakati ili kuepuka masaibu.

Hata hivyo ni afueni kwa wakulima wanaoendesha kilimo hasa cha upanzi wa mimea mbalimbali  kwani  kwa sasa wamebahatika kuweza kupata ratiba nzuri ya jinsi wanastahili kujipanga  kwa kilimo ili kuhakikisha kuwa  hamna lolote liendalo kwa ubaya.