Mshauri wa rais

Aliyekuwa mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria  na mshauri wa serikali amejutia tabia  na mienendo ya wanasiasa nchini. 

Kuria katika matamshi  yake kwenye X aliweza kuelezea kusikitishwa  kwake  na hatua  ya wanasiasa nchini kuchukua  mkondo mbaya wa kuwakejeli walimu nchini.

''Kuna maono mengi kuhusu jinsi ya kuangamiza  taifa lakini  kwa  yale  ambayo yanaonekana na kuwa ya  mvuto mkuu ni ya wanasiasa kupanga misururu ya fomu za kuwaajiri walimu katika mikutano ya hadhara na ya umma.

Hilo ni jambo la kusikitisha sana hasahasa kwetu kama viongozi amba o tumepiitia kwa walimu ambao tuanaonekana kuwakejeli licha  ya kupata manufa makuu  kutoka kwao, hapo tumejishusha sana'' Mosese Kuria alieleza.

Katika siku za hivi majuzi, baadhi ya wabunge walionekana wakichukulia  suala la walimu kuajiriwa kama suala  la kisiasa bila kufahamu kuwa ni suala ambalo huwa chini ya tume ya  kuwajiri walimu TSC Nchini. 

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kulingana na usemi wa katibu mkuu wa tume ya kutetea masilahi ya  walimu KNUT  Bwana Collins Oyuu aliweza kuwakosoa wabunge kwa kuweka mbele  masilahi yao na kuikosea heshima  tume  ya kuwaajiri walimu TSC kwa kulichukulia hilo swala la walimu  kuajiriwa kama mchezo wa paka na panya.

Oyuu alisikitikia pakubwa mienendo na tabia ambazo zimekuwa zikichuliwa na wanasiasa kwa  kutembea  na fomu za kuwajiri walimu kwa  kuwaamuru kupanga foleni  akisema kuwa  ni jambo la aibu sana.

''Inasikitisha na  inaudhi kuweza  kuona  taasinia ya ualimu ikidharauliwa kiwango cha kuweza  kuwaruhusu wanasiasa  kuchekea taaluma  hii muhimu kwa kushinda wakiwaamuru watu kupanga foleni  katika matanga na kwa sababu ya kutaka kupata sifa na  imani kutoka  kwa wananchi.

 Walimu wanapohitajika kuajiriwa au kupandishwa cheo  hilo ni jukumu ambalo liko katika katiba ya Kenya na inastahili kuheshimiwa Ambapo ni jukumu la TSC si mtu binafsi.

Kama muungano wa walimu tungependa kulani tukio hilo la aibu ambapo wabunge tena watunga sheria wetu katika bunge la taifa wanafahamu kile ambacho kinastahili kuwa kikijiri kwa ustaarabu mkuu tena wa kisheria ifaavyo'' bwana Oyuu  alieleza.

Wabunge kadhaa walionekana wakiwaeleza  wananchi katika hafla za mikutano kuhusu uwezo wao wa kuwapa kandarasi za kudumu za kazi ya uaalimu bila  ubaguzi wala upendeleo wowote.