
Timu ya Kenya ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Rising Stars, iliondoka Jumatatu asubuhi kuelekea Misri kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2025 itakayofanyika nchini Misri.
Haya yanajiri siku moja baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kutangaza tarehe, muda wa kuanza na maeneo ya makundi na hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
Makala ya 17 ya michuano hiyo itaanza Aprili 27 na kuhitimishwa Mei 18. Mataifa 13 yatachuana katika viwanja vitatu vya Cairo, Ismailia na Suez.
Mechi ya ufunguzi itafanyika Jumapili, Aprili 27 huku wenyeji Misri wakikabiliana na Zambia kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Mapema jioni hiyo, Sierra Leone itamenyana na Afrika Kusini katika Kundi A huko Ismailia.
Nigeria na Kenya zitafungua dimba la Kundi B Mei 1 kwenye Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo, na kufuatiwa na Kenya dhidi ya Morocco katika uwanja huo huo.
Senegal itaanza kutetea taji lake dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mechi ya ufunguzi ya Kundi C mnamo Mei 2 huko Suez kabla ya DR Congo kumenyana na Ghana katika uwanja huo huo baadaye.
Mashindano hayo yatafuata muundo wa makundi matatu. Kundi A lina timu tano. Kundi B na C lina timu nne kila moja.
Timu mbili za juu kutoka kwa kila kundi, pamoja na timu mbili bora zilizoshika nafasi ya tatu, zitafuzu hadi robo-fainali.
Washindi wanne wa nusu fainali watafuzu kuwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia la FIFA Chile 2025, kuendeleza utamaduni wa bara la Afrika wa ubora wa kimataifa katika soka ya vijana.
Makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika la Vijana chini ya umri wa miaka 20 ya CAF, Misri 2025
Kundi A: Misri, Zambia, Sierra Leone, Afrika Kusini, Tanzania
Kundi B: Nigeria, Tunisia, Kenya, Morocco
Kundi C: Senegal, Jamhuri ya Afrika ya Kati, DR Congo, Ghana
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!