Simba

Msichana mwenye umri wa miaka 14 alifariki dunia baada ya kushambuliwa na simba wa kike katika tukio la kutisha karibu na Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, tukio linaloangazia hatari inayoongezeka ya migogoro kati ya binadamu na wanyama pori nchini Kenya.

Shambulizi hilo lilitokea kwenye shamba lililozunguka upande wa kusini wa hifadhi hiyo, ambapo mamlaka zilithibitisha kuwa msichana huyo alikuwa ndani ya maeneo ya shamba hilo wakati alipo shambuliwa.

Hata hivyo, maelezo kuhusu mazingira ya shambulizi hili bado ni machache, na Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hili.

Shirika hilo limetoa hakikisho kwa umma kuwa taarifa zaidi zitapatikana mara uchunguzi utakapo kamilika.

Tukio hili linajiri baada ya tukio lingine la kutisha ambapo mwanaume mwenye umri wa miaka 54 aliuawa na tembo katika Kaunti ya Nyeri. KWS ilieleza pole zake kwa familia za waathirika, ikitambua athari kubwa za vifo hivi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ili kukabiliana na hali hii, KWS imepeleka timu za dharura kwenye maeneo yote mawili ili kudhibiti hali na kuzuia mashambulizi zaidi. Shirika hilo pia linahimiza uangalizi mkubwa na utayari katika maeneo yaliyo hatarini kwa migogoro ya binadamu na wanyama pori.

Mwelekeo huu wa migogoro, hasa katika jamii zinazokaribu na maeneo ya hifadhi, unaendelea kuwa changamoto kubwa. 

Maafisa wa hifadhi i na viongozi wa jamii wanasisitiza haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuboresha uzio, mifumo bora ya tahadhari mapema, na kuongezeka kwa elimu ya umma ili kupunguza hatari hizi na kulinda maisha ya binadamu na wanyama pori.