Police vehicle

Washukiwa wawili walikamatwa na makachero wa DCI kwa kujifanya kuwa walikuwa wanatoa huduma za ukandaji wa mwili.

Washukiwa hao wawili walikamatwa na makachero wa DCI katika  kituo  cha Kasarani kwa tuhuma za kuendeleza  matangazo katika mitandao ya kijamii kuwa walikuwa wanatoa huduma za kukanda miili ya binadamu.

Washukiwa hao wawili  walionyesha ujuzi  mkubwa wa  kazi yao katika mitandao wakiwa wamejipodoa vizuri na kuwavutia wanaume pamoja na wateja wa kike kwa jumla.

Katika harakati za kuhakikisha kuwa wanawashughulikia wateja wao walikuwa wakiwaibia kila kitu ambacho wateja walikuja nacho pamoja na pesa hivyo kuhatarisha  maisha yao.

Watu wengi wamepitai  katika hali hiyo ya unyama kutoka kwa washukiwa hao ambao ilisemekana walikuwa wakiendeleza  biashara yao kwa   muda mrefu bila kukamatwa kabla ya hila  zao kugunduliwa na maafisa wa usalama.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwathiriwa mmoja aliweza kuripoti tukio hilo kwa maafisa wa  polisi katika kituo  cha Kasarani ambapo uchuunguzi wa kina kuwahusu  ulianzishwa na hatimaye nyama  ya hao wangwana ilifichuka.

Washukiwa hawa wamekuwa wakiendeleza shughuli hiyo  wakiwa katika mtaa wa Lumumba Drive eneo  la Kasarani jijini Nairobi huku wakiwa wamewahujumu raia wengi na hiyo biashara yao ya utapeli.

Katika kisa  kimoja kilichosababisha   wao kukamatwa ni kuwa waliweza kumwalika mteja mmoja ambapo  alimpeleka katika chumba chao cha kutoa  huduma za kukanda mwili ambapo walifanikisha shughuli zao  kisha kabla ya kutamatisha waliweza kutoa visu vikali na kumwelekezea mteja wao huku wakimtishia maisha tayari kwa  kumuua.

 Kutokana na hali  ya uwoga na kutaka kuokoa  maisha yake  mteja huyo aliwapa kibali cha kupokea pesa ambapo walimlazimisha kutoa shilingi 280,000  kisha wakachukua vifaa vyake vya thamani hatimaye wakamrusha  nje  ya chumba.

DCI waliweza kusema na kutangaza kwa kuanzisha uchunguzi wakina tena wa undani zaidi ili kuweza  kutambua matapeli wengi ambao wamekuwa na hiyo hulka  na tabia ya kuwatapeli  watu  wengine kwa kutumia njia  hizo za  hila na ujanja.

Washukiwa  hao waliweza kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kamiti na gereza la kamiti ambapo wanazidi kupunga unyunyu huko wakitumia hela hizo alizoiba huku polisi wakiendeleza  juhudi za  kukamilisha uchunguzi na Kuwafikisha kortini kwa mashitaka.