Chuo kikuu cha Bomet

Mahafali wa chuo kikuu cha Bomet katika kaunti ya Bomet walalamikia ucheleweshaji wa kutoa vyeti vyao.

Mahafali  hao walilalamika wakisema  kuwa chuo kimechukua muda mwingi kuweza kuwapa vyeti vyao vya masomo licha ya kutamatisha masomo yao kwa muda  wa miezi minne iliyopita.

Wanafunzi hao waliofuzu mwaka jana  Disemba walisema kuwa walipewa vyeti vya kuhitimu kutoka kwa  shule ila hawajapewa cheti cha masomo mbalimbali yaliokuwa wakifanya.

Walisema  kuwa matokeo ya kila somo  ni muhimu sana  kwa maana waajiri huko nje husisitiza kwa kutaka kuona  jinsi mwanafunzi alivyokuwa  akifauli katika   masomo yake.

Kulingana  na usemi wa  wanafunzi  hao  walisema kuwa chuo kilikuwa kimekwamilia stakabadhi hizo za  masomo kwa  misingi kuwa   kulikuwepo  na hitilafu za  kimitambo  jambo ambalo lilichochea  kukawia kupatikana kwa cheti hicho cha  kuonyesha  masomo mbalimbali.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wanafunzi walilalama wakisema kuwa walikuwa  wakipoteza nafasi muhimu sana za ajira kutokana na  kukosa  cheti  hicho muhimu  ambacho kimekuwa kikiitishwa na waajiri.

Chuo cha  Bomet kiliasisiwa kupitia kwa notisi ya sheria nambari 145 mnamo 27 Julai, 2017 kuweza kuhudumu kama chuo mbadala kutoka chuo kikuu cha Moi.

Chuo hicho cha Bomet kimejiweka katika nafasi ya kuhudumu kama chuo ambacho kinajihusisha pakubwa na masomo tekelezi katika nyanja ya Teknohama na Mabadiliko , udhibiti wa mazingira  na maendeleo ya  ujasiriamali.

Wanafunzi waliweza kusisitiza  kwa kusema  kuwa chuo kukosa kutoa rekodi nzuri ya hali ya masomo katika chuo hicho hiyo inatishia na kuweka  maisha  ya masomo yao katika   hali ya hatari kwa sababu ya kukosa kupata stakabadhi muhimu za masomo kwa wakati.

Licha ya chuo kusisitiza na kutangaza kuwa  kiko imara kwa  kutoa mafunzo tekelezi katika nyanja mbalimbali na kwa kudhihirisha kuwa mambo haya yanafanikishiwa ni lazima chuo kiweze kuweka misingi imara tena dhabiti kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi hawapati wakati   mgumu wakati wa na baada ya kutamatisha  masomo yao.

Huwa ni furaha kwa mzazi pamoja na mwanafunzi kuhitimisha masomo yake  kisha kufanikiwa kwa kupata ajira hiyo huwa ni jambo la kufurahia na huleta shangwe kwa jamii.