RAIS WILLIAM RUTO

Rais  Ruto alikariri kwa kusema kuwa  bima ya afya kwa  wote alimaarufu UHC ilikuwa sawa na ya manufaa  kwa wakenya.

Rais  Ruto alisema hayo alipokuwa katika ikulu ya Nairobi  siku ya Alihamisi 17,Aprili 2025 alipokuwa katika hafla ya  kuwaapisha mawaziri walioteuliwa na waliopigwa na  msasa na bunge la taifa na kupitishwa  na bunge.

Rais  alisisitiza  kuwa taifa lilikuwa  limejaribu kuendesha mfumo  wa matibabu  nchini Kenya akisema kuwa kwa  serikali zilizopita  zilijaribu kwa hatua kubwa kufanikisha mpango  huo. 

Rais  alisema kuwa uongozi uliopita  ulifanya bidii na jitihada kuhakikisha kuwa angalau mfumo huo unafanikiwa lakini kwa  namna moja au nyingine malengo lengwa hayakuafikiwa.

Rais  alisema kuwa aliyekuwa waziri wa Afya Charity  Ngilu pamojana profesa Anyang' nyong'o walijaribu kaddri ya uwezo waxo kufanikisha mpan go wa bima ya afya kwa wote   ikiwemo serikali ya  Jubilee  ila ufanisi ulikuwa finyu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 Rais alisema kwa  wazi kuwa  wakati sasa ulikuwa umewadia kwa kuweza kufanikisha  mpango huo akisema kuwa  mara  hii itawezekana kwa kuwa ukuruba uliopo kati  ya serikali ya Kenya  kwanza  pamoja  na wanachama  kutoka vyama vingine vya upinzani kwa serikali jumuishi .

Ruto alisema kuwa alikuwa  na matumaini makubwa  kuwa ushirikiano uliopo wa  kisiasa kwa  sasa ni ushirikiano amb ao utawezesha kila jambo na ahadi za serikali kutimia .

  Kulingana na mujibu wa usemi wa Rais  Ruto idadi ya watu au wakenya ambao walikuwa wakijiunga  na bima hiyo ya UHC ilikuwa  ya juu  sana akisema kuwa jumla ya watu 50,000 huwa wanajisajili katika  bima  hiyo  kwa siku  kuashiria kuwa maendeleo makubwa  yalikuwa yakionekana. 

Vilevile  Rais alisema  kuwa alikuwa akipokea usemi kutoka kwa  marafiki,wanajamii, watu aliosoma nao  pamoja na wakenya kutoka matabaka mbalimbali kuhusu  jinsi mpango wa  UHC ulikuwa umewasaidia pakubwa kuweza kulipa bili za  hospitalini na vilevile  kuwapa wakati mwepesi kufanikisha na kuendeleza shughuli zao bila matata yoyote.

 Rais  alisema  kuwa bima  hiyo  itawasidia wakenya wote kuweza  kupata matibabu na wala si kama awali ambapo watu wachache ndio waliokuwa wakinufaika pakubwa huku wengi wakihangaika  kwa  kuuza  mali zao kwa sababu ya matibabu.