
Mfanyabiasha mmoja anayedaiwa kuendeleza biashara ya uuzaji wa magari akabiliwa na tuhuma za kutolipa ushuru.
Mfanyabiashara huyo mwanzoni aliyeripotiwa kwenye asasi za uongozi na akalazimika kusitisha biashara hiyo imebainika kuwa tena ameifufua biashara hiyo na kuipa jina jipya.
Kulingana na baadhi ya wateja wa huyo mfanyabiashara inasemekana kuwa alikuwa akiwaahidi wateja wake kwa kuwauzia magari huku baada ya malipo kufanyika kuna muda mwingi wa kuwasilisha gari hilo kwa mteja husika.
Ilisemekana kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa na mazoea ya kuchelewesha uwasilishaji wa magari kwa wateja wake sababu kuu ikiwa ni kuwa mfanyabiashara huyo wa magari alikuwa anatumia njia ya mkato kupitisha magari katika bandari ya Mombasa kwa kutolipa ushuru ifaavyo.
Mshukiwa huyo ambaye ana biashara ya umiliki wa magari kwa jina House of Cars iliyo katika vichorochoro vya Jobavu Nairobi mwanzoni aliwahi kuhusishwa na kampuni ya magari ya Kheng Kheng ambayo inadiwa kuwa ilibadilisha jina ila huduma zake zilisalia zilezile.
Katika msururru wa matukio ya arafa mteja mmoja alimshutumu mfanyabiashra huyo kwa kuweka kiasi cha shilingi milioni 3.95 Agosti Mwaka jana 2024 kwa ajili ya kununua na kumpokeza gari aina ya Toyota Prado ila hakuwasilisha gari kwa mteja wake miezi kadhaa baadaye.
Alisema kuwa angemrudishia mteja wake pesa Januari mwaka huu 2025 ila pesa hizo kufikia sasa hazijarudishwa. jambo lililosababisha mlalamishi kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Muthaiga.
Hata baada ya hapo hakuna lolote la ziada ambalo limefaaanyika kufanikisha upatikanaji wa haki upande wake licha ya kuendelea kulipa mkopo wa benki kutoka kwa Benki ya NCBA kulipa hela hizo.
Kuna madai kuwa mfanyabiashara huyu huwa na ukuruba na ushirikiano wa karibu sana na maafisa wa bandarini Mombasa ambao humsaidia kuweza kukwepa ulipaji wa ushuru kwa KRA Pamoja na kusitisha huduma zote zinazohusiana na uagizaji wa magari kwa wateja wake baada ya wateja kulipa.
Hata hivyo umma umeombwa kuwa macho na makini wanapofanya ushirikiano wa kibiashara na mfanyabiashara huyo kwa ajili ya usalama wao.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!