
Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen alishirika katika mkutano wa usalama wa uchimbaji wa madini.Ni mkutano uliofanyika tarehe 16 Aprili, 2025 jijini Nairobi.
'' Idara ya uchimbaji madini ni muhimu tena huchangia pakubwa katika ukuuzi wa uchumi wa nchi ila kuwezesha asasi za kulinda usalama kutulia pasi kuangazia usalama wa hali hiyo ambapo ni hatari.
Makuuzi ya nyanja hiyo yamenyamaa na kuvuvia kutokana na uchimbaji wa madini ambao si halali na ambao unasitahili kudhibitiwa na kuwekwa katika shajara ya serikali'' Murkomen alieleza.
Kando na kupoteza mapato pamoja na kupata kiwango cha chini cha wawekezaji ambao ni waaminifu, uchimbaji wa madini ambao si halali pia huweza kuharibu mazingra, kuleta vita kung'ang'aniwa kwa raslimali, hali ya afya kuwa mbaya, ajira kwa watoto wadogo na usalama kuhusu wananchi.
Kulingana na mwelekeo wa huduma ya polisi kwa taifa pamoja na kampeni endelavu ya jukwaa la usalama ukanda wa Pwani hayo ni baadhi ya masuala ambayo yalikwa yanaikumba wizara na idara ya uchimbaji madini nchini.
Kutokana na hayo wizara ya usalama iliazimia kufanya mabadiliko katika idara ya madini kwa kuwaongezea maafisa wa usalama ambao watakuwa na jukumu la kutahimini jamii kwa kuangazia ni wapi zoezi la uchimbaji madini litakuwa likiendelea pamoja na kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inafanikishwa kwa usalama kwa kuwepo kwa usalama wa taifa.
Waziri Murkomen alikuwa ameandaa mkutano huo uliowaleta pamoja washikadaau wote katika wizara zote mbili wizara ya usalama na wizara ya uchimbaji wa madini iliku boresha shughuli hiyo muhimu.
Maafisa waliohudhuria mkutano huo wa pamoja ni waziri wa uchimbaji madini na uchumi wa majini waziri Hassan Joho, katibu mkuu katika idara ya uchimbji wa madini Harry Kimtai, inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, Naibu afisa mkuu wa polisi Eliud Lagat naibu insipekta mkuu wa polisi Gilbert Masengeli, mkurugenzi mkuu wa DCI Mohamed Amin miongoni mwa maafisa wengine wa usalama.
Mkutano huo ulipania kutoa suluhisho kuhusu uchimbaji wa madini na kuhakikisha kuwa iwapo shughuli hio inatekelezwa inaafikia viwango hitajika vya kisheria.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!