DOUGLAS KANJA

Huduma ya Polisi kwa  umma ilitoa  taarifa rasmi kuhusiana na operesheni ya Polisi inayoendelea Haiti.

Huduma  hiyo  ya taifa ya polisi  iliweza kusema kuwa iliweza kuona habari zilizokuwa zikisambaa katika gazeti la Daily Nation la tarehe 15, Aprili,2025 lililokuwa  likitilia shaka ufaafu wa  maafisa  wetu katika operesheni ya kijeshi nchini Haiti.

Huduma hiyo ilisema kuwa ilipinga vikali na kulaani habari hizo ikizitaja kama zisizo za kweli na ambazo zimekosa uzalendo wa taifa.

 Huduma  hiyo ya polisi iliweza  kusema kuwa utoaji wa maafisa  hao wa polisi kuenda katika taifa la Haiti  kwa  ajili ya Operesheni ni kutokana na maafikiano  ya umoja wa mataifa kuhusu kusuluhisha masuala na vita na upatikanaji wa amani katika nambari 2699 ya mwaka 2023.

 Kutokana na maafikiano hayo ndipo maamuzi ya Kenya kuweza  kutoa usaidizi kwa taifa la Haiti ili kuweza kuhakikisha,usalama unaafikiwa kwa  taifa hilo la Haiti ambalo limekumbwa  na maasi kutoka kwa magaidi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kulingana na  ripoti ya  Huduma ya  polisi ilisema kuwa polisi walikuwa wamepewa kazi mafunzo ya kutosha kuhusu jinsi ya kutumia  mambo kadhaa yakiwemo utumizi wa Bunduki maalum za  vita.

Vilevile walikuwa wamejifunza jinsi ya kudhibiti umma kwa kiwango cha juu, sheria za  kimataifa na  sheria  na  haki za  binadamu, polisi  waliweza kujifunza jinsi ya kulinda amani na vilevile kujifunza jinsi ya kuzungumza Lugha ya Kifaransa.

 Huduma ya Polisi iliweza kusema kuwa kwa kuzingatia mafunzo hayo yaliweza kuwapa  nafasi ya kuweza kuendeleza  huduma zao za operesheni bila  matata yoyote.

Maafisa waliweza kupewa magari ya spesheli ya kivita kama vile MRAPS, balistiki Helimeti, nguo za karandinga na  jinsi ya  pamoja na vifaa  ambavyo vinawasaidia kuweza kuhakikisha kuwa kila kitu kiko  shwari ni ajili ya kupambana na operesheni hiyo.

Kulinganna na ripoti ya usalama wa  kimataifa ambayo Kenya imekuwa ikishiriki ilikuwa wazi kuwa wangefanikisha operesheni hiyo  kwa  kuhakikisha  kuwa wanafaniksha misheni hiyo maaluum bila kutatizika.

Kutokana na   historia pana  tena yenye ufanisi mkubwa  ambayo Polisi Wa Kenya wameshiriki  ni kuhakikisha kuwa  kila kitu kinafaulu na  kwa  kufaulisha shugul hiyo ya usalama Haiti hiyo ni kuipa sifa taifa la  Kenya  Pamoja na umoja wa kimataifa.