Mkutano wa kuangazia mabadiliko ya tabianchi Kenya na Ufaransa

Waziri wa mazingira na misitu Deborah Barasa alihudhuria kikao cha pamoja na ubalozi wa  ufaranja ili kujadili masuala muhimu ya mazingira jijini Nairobi.

'' Nimeshiriki mazungumzo na wajumbe  katika mkutano wa kimataifa na balozi wa Ufaranja Agnes Pannier Runacher pamoja na  waziri wa  masuala ya maisha ya vimelea  vya  ardhini pamoja na maisha ya  mazingira yanayowazunguka wanyama hao.

Vilevile kulikuwepo na mabadiliko ya misimu, misitu,na wanyama wa majini na uvuvi, ambapo mazungumzo yalijikita pakubwa katika kuimarisha mabadiliko ya tabianchi  duniani  kuongeza na kuzamia  katika mabadiliko ya tabianchi duniani'' Debora alieleza.

Huo mkutano ulijiri wakati ambapo kunatarajiwa kuwa na mkutano wa kimataifa kuhusu mipango na mikakati ya kuwa na mazingira mema alimaarufu UNFCCC COP30 mji wa Belem Brazil  kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na usawa kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na mazingira mazuri pamoja na tabianchi ambayo ni sawa kote Afrika.

Ushirikiano wa taifa la Kenya na Ufaransa uliafikia  ufanisi mkubwa katika kuhakikisha kuwa kunajengeka mifumo imara tena dhabiti kuhusu mwendelezo kuhusu masuala ya tabianchi,ambapo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na  kujengeka  kwa  mazingira ambayo ni  mwanzo wa kuimarisha uhusiano mwema wa kimataifa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika Mkutano huo kulikuwepo na balozi kutoka taifa la Ufaransa Kenya Arnaud Suquet, Katibu mkuu katika masuala ya mazingira , Bwana Gitonga Mugambi wa Misitu,Betsy Njagi wa uchumi wa  majini  miongoni mwa viongozi wengine wengi.

Masuala ya mazingira hasa katika suala la Tabianchi limekuwa likizungumziwa sana kwa muda mrefu  huku  mataifa yote  yakiwa na  rai  kuwa angalau kuwe  na ushirikiano wa karibu ili kuepuka kuharibu  mazingira haya ya tabianchi. 

Taifa  la kenya limekuwa likishniriki  katika makongamano kadhaa kuhusiana  na  masuala ya tabianchni ili  kuhakikisha  kuwa kuna  ufanisi wa  kipekee kwa kujenga na kuwa  na mazingira  ambayo ni  salama kwa mataifa  yote.

 Mataifa ya Afrika  yamekuwa yakitoa wito kwa mataifa ya ulaya kuweza  kufidia au kuongza  kiwango  cha kutoa pesa kwa ushikiano wa kidunia wa kulinda mazingira ya tabianchi kwa  kusema kuwa  mara  nyingi yamekuwa yakiharibu mazingira kwa kutoa gesi chafu kwa wingi.