
Kiongozi wa chama cha DAP Kenya Eugene Wamalwa alisema kuwa wanafunzi walikuwa wakiwasilisha ujumbe muhimu kwa Wakenya kupitia kwa mchezo wa kuigiza.
Wamalwa alikuwa akirejelea matukio yaliofanyika mnamo Alihamisi 10 Aprili, 2025 katika Kaunti ya Nakuru ambapo wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Butere walizuiwa na maafisa wa usalama kuweza kuigiza mchezo wao wa Echoes of War.
Alikuwa akizungumza katika kituo cha Runinga cha NTV asubuhi wakati alipoulizwa aelezee msimamo wake kuhusu tukio hilo lililojiri katika Kaunti ya Nakuru.
Wamalwa alisema kuwa Maudhui ambayo yalikuwa yamebebwa katika mchezo huo yalikuwa ni masuala ambayo yalifaa kusikilizwa na kutazamwa na wakenya pamoja na wananchi ili waweze kusikiliza na kujitathimini ipasavyo.
Kulingana na matamshi ya mheshimiwa Wamalwa alisema kuwa serikali ilikuwa imesusia kadamnasi na peupe kuwasikiliza viongozi kutoka matabaka mbalimbli wakiowemo viongozi wa dini kuhusu hali halisi ya matibabu na hali ya uchumi nchini.
'' Mwanzo kabisa wacha nianze kwa kuwapongeza na kuwashukuru wanafunzi kutoka shule ya upili ya Butere kwa kuonyesha ujasiri wa kipekee katika harakati na pilikapilika za kuhakikisa kuwa wanafahamisha umma kuhusu ukweli ambao unatusonga kama taifa.
Wanafunzi walikuwa na ujumbe mwema wa kumwarifu rais kuwa alikuwa uchi kutokana na masuala ambayo yalikuwa yanafanyika nchini kuhusu mambo ya Ukosefu wa ajira, Hali ngumu ya maisha ,utekaji nyara, utozaji wa ushuru wa juu kwa wakenya miongoni mwa masuala ambayo yallikuwa yakiwaathirii wakenya kama suala la Bima ya matibabu ya SHA.
Wamalwa alisema kuwa huo ujumbe ulikuwa umebeba mambo ambayo rais angesikiliza na kutazama angelikuwa na wakati mwema wa kuyashughulikia kwa sababu washauri wa kike pamoja na wale watu ambao walikuwa karibu na yeye walikuwwa wamemwangusha kwa kutomshauri na kumweleza ukweli wa Mambao jin si inavyo faa'' Wamalwa alisema.
Katika usemi wake Eugene alisema kuwa katika enzi zake akiwa shuleni alikuwa mwana drama na aliweza kuwasilisha michezo ya kuigiza mbele ya rais Moi moja kwa moja wapo ikiwemo ya kupinga madhila na dhuluma Moi alikuwa akizielekeza kwa wananchi enzi zake.
Vilevile Eugine Alishangaa ni kwa nini mama wa Taifa Bi Rachael Ruto alisalia kimya kuhusu hilo suala la shule ya B utere ilihali ilikuwa shule yake ya zamani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!