Education CS Julius Ogamba / FIle

Wizara ya elimu ilitoa taarifa kamili kuhusu hali ya mchezo wao wa  kuigizwa wa ''Echoes of  War''.tamthilia ya drama ya wanafunzi wa shule ya upili ya Wasichana ya Butere 

Ni mchezo uliotarajiwa kuigizwa katika mashindno ya kitaifa  katika kaunti ya Nakuru mnamo Aprili 10, 2025.

''Shule  ya kitaifa ya wasichana ya Butere  inapatikana  katika   gatuzi  la Kakamega na inajulikana kwa ujuzi  wa kipekee kwa kuunda drama za kipekee na za  kuvutia kote  nchini hasa  katika michezo ya kuigizwa.

Mchezo wa kuigizwa mwaka huu katika mashindano ya Drama uliopewa jina Echoes of War  uliweza kuleta hali ya  sin tofahamu na mwingiliano  wa  vita kati  ya serikali na shule hiyo kutokana na  maudhui ya  mchezo huo  na  asasi za  sera za   usalama wa taifa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wakati ambapo mchezo huo ulipoigizwa katika kiwango cha eneobunge waamuzi  wa mashindano hayo  waliamueleza  mwandishi wa mswaada  huo kuondoa  baadhi ya vifungu ambavyo vinaleta mkinzano wa kimasilahi barua ilifafanua.

Katika kiwango cha  Kaunti mchezo huo wa  kuigizwa haukukuwa na  athari zozote  wala usemi mbaya na uliamuliwa uweze kusonga katika kiwango cha mkoa, katika kiwango cha  mkoa mswada wa mchezo huo ,uliweza kuongezwa maneno mengine ya  uhasama ndani yake.

Kwa  kuweza  kubaini hilo kuwa  mswada uliweza kuongezwa maneno mengine  usimamizi wa shule uliafikia uamuzi kuwa  mchezo huo usichezwe katika kiwango  cha kitaifa kwa  kuwa ungeleta masuala  ya ukinzani na sera za serikali.

Sheria  ya udhibiti namb ri 19.2 ya  sheria  za drama  inasema kuwa mageuzi yoyote katika  mswada wa uigizaji ni lazima uwe mdogo  sana na  iwapo utafanya mabadiliko  bila wakaguzi na waamuzi kujua bila shaka mswada huo utaweza  kufutiliwa  mbali.

Shule  kubaini kuwa mswada huo ulikuwa umebadilishwa kwa namna moja au  nyingine shule haikupeleka ukaguzi wa mswada huo kwa katibu mkuu wa usimamizi wa ngazi ya maeneo kwa ukaguzi na ukubalisho.

 Kama ilivyo ada  ya sheria ni kuwa  iwapo  mswada wa uigizwaji   unakosa kufanyiwa  ukaguzi  katika hicho kiwango cha  mkoa  bila shaka  unatemwa nje kulingana na sheria.

 Hata  hivyo Mahakama moja  Kisii na nyingine maeneo ya Kakamega zilikuwa  zimetoa amri  ya kuwaruhusu wanafunzi hoa kuendelea na uigizaji wa tamthilia  yao ya ECHOES OF WAR.

Ila  kulingana  na  sheria za Muziki na Drama hairuhusiwi mtu wa nje kando na mamlaka  ya shule  kuweza  kuendeleza ukufunzi wowote kwa kisingizio  kuwa ni mwelekezi wa michezo ya  kuigiza. 

Kwa hivyo kujihusisha  kwa  Cleophas Malala katika mchezo huo wa  kuigizwa ilikuwa ni kinyume  cha sheria za Drama na muziki kulingana na kifungu  nambari 9 (c)cha sheria za Drama'' wizara ya elimu ilitoa maelezo hayo kupitia kwa barua rasmi.