
Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ameshiriki mkutano wa pamoja na wakulima wa makadamia katika kaunti ya Meru.
Ni mkutano ambao uliweza kuwaleta pamoja wakulima pamoja na waziri ili kujadili jinsi ya kuimarisha kilimo hicho na kufanikisha mpango maalum wa kuen deleza kilimo mashinani.
Wakulima waliweza kuelezea changamoto ambazo wamekua wakipitia hasahasa zao la miraa, kulingana na usemi wa wakulima hao waliweza kusema kuwa wamekuwa wakipitia changamoto tele kutokana na kupata hasara ya zao la makadamia miongoni mwa mazao mengine.Mazao kutoka kwa viongozi hao ambao waliweza kujumuisha mazao hayo ili kuwaza kupata suhuhu la kudumu.
Wakulima hao ambao wako katika miungano mbalimbali ya ukulima wa mazao ya makadamia, avokado, kahawa, na miraa, Kulingana na wakulima hao waliweza kuwa na uchuu kuweza kuwasilisha lalama kuhusiana na matatizo kuhusu matatizo ya makadamia na kilimo kwa jumla.
''Mimi ninasimama hapa kwa kusema kuwa soko la makadamia limepungua bei sana mwanzoni kulikuwa na soko zuri kwa kilo moja ya makadamia iilikuwa ni shilingi 250 lakini siku hizi makadamia yanatoka shilingi 100 hadi 80 kwa kilo jambo ambalo linaumiza mkulima sana hata wengine huuza shilingi 40 kwa kilo.
Mheshimiwa tukiwa hapa Meru kuna jambo ambalo tunakuomba utusaidie kuhakikisha kuwa tunapanga na kuimarisha bei nzuri ya makadamia kwa wakulima tunataka kuhakikisha kuwa unatusaidia kuhakiksha kuwa tunatatua shida hii ya Makadamia tunataka utusaidie tukishirikiana na muungano wa wakulima wa AFA'' mwenyekiti wa wakulima wa Makadamia alieleza.
Mkulima mmoja aliweza kusema kuwa tatizo la kuzorota kwa bei ya makadamia ni kutokana na kampuni nyingi za kusaga na kupakia bidhaa za mwisho ambapo hizi kampuni zimekuwa zikiharibu bei ya makadamia kwa kumpunza mkulima kwa kuwafinyilia chini kwa ajili ya bei.
Shirika la AFA(AGRICULTURE AND FOOD AUTHORITY) ni shirika la serikali ambalo lina wajibu wa kuwaelekeza wakulima jinsi ya kuendeleza mazao ya ukulima kwa kuwapa mbegu murwa na kuhakikisha kuwa wakulima hawatapeliwi na vilevile kuwatafutia soko maalum.
Shirika hilo la AFA liko na jukumu la kuhakikisha kuwa mkulima anahakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sambamba ili kuimarisha hitaji la mkulima na vilio vyao ili kuhakikisha kuwa kila jambo ni la kuimarisha vyema.
Kumekuwa na matatizo ya wakulima kuuziwa makadamia ambayo ni ghushi huku jukumu la kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika kwa kupata mbegu sahihi kwa ajili ya kupata mbegu nzuri.
Waziri aliweza kuzuru ili kuweza kusikiliza malalamishi ya wakulima kwa ajili ya kupata suluhisho la kudumu jinsi ambavyo watapata malalamishi yao.
AFA ni shirika la serikali ambalo linahusika na maz ya pamba, mira, pareto, viazi, makadamia,miraa,avocado, maua, majanichai na kadhaalika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!