Afisi ya insipekta mkuu wa polisi ilitoa taarifa kamili kuhusiana na matukio ya Drama katika Kaunti ya Nakuru kuhusiana na Shule ya Upili ya wasichana ya Butere.
''Huduma ya polisi ya taifa ambayo inatambulikana katika kifungu nambari 244 cha katiba ni moja kati ya hitaji muhimu la usalama ni nguzo muhimu ya usalama ambayo ina jukumu la kulinda na kudhibiti mali na maisha ya wananchi bila kuvunja haki za wananchi.
Huduma hii ya polisi ina jukumu kuu la kuhakikisha kuwa inalinda huduma zote za michezo katika mashindano ya drama kwa shule za upili na vyuo vikuu katika kiwango cha kitaifa kwa kuhakikisha kuwa shughuli iyo inafanikishwa bila vizingiti vyovyote.
Mnamo siku ya Alihamisi 10, Aprili, 2025 tulipokea habari za kijasusi za kuaminika kuwa kulikuwa na watu ambao walikuwa wanapanga kusambaratisha mashindano hayo ya sherehe na kama huduma ambayo ina wajibu wa kuhakikisha kuwa usalama unakuwepo tuko imara na mstari wa mbele kuweka mikakati ya usalama ili kuzuia mpango huo.
Hata hivyo kuna madai kulikuwa na matukio ya matumizi mabaya ya mamlaka kutoka kwa baadhi ya maafisa wetu wa usalama waliopelekwa huko Nakuru kwa ajili ya kuhakikisha kuwa usalama una dumishwa ipasvyo.
Inspekta mkuu wa polisi aliweza kuamurisha uchunguzi wa haraka wa madai hayo kwa maafisa wa polisi ambao kwa namna moja au nyingine waliweza kuhusika katika mienendo mibaya ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Afisi ya inispekta wa polisi iliweza kutangaza kwa kusema kuwa vitengo maalum ambavyo vinashughulikia masuala ya huduma za polisi kama IPOA pamoja na kikosi cha kuchunguza masuala ya ndani kiweze kufanya uchungunzi wa kina kuhusu maadai hayo na kutoa ripoti chini ya siku 21 zijazo.
Huduma ya polisi inajitoa kwa kuhakikisha kuwa inatoa huduma za usalama kwa uwazi , uwaminifu na kwa kuzingatia katiba bila kuwa na muegemeo wowote wa kisiasa bali kwa kuzingatia sheria na kutii na vilevile inaruhusu uhuru wa kunjieleza kwa kila mmoja pamoja na kutangamana bila vizuizi'' mwisho wa nukuu ya barua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!