
Manaibu Gavana wasisitiza kutengewa bajeti yao kando ili kuendeleza kamati mbalimbali katika Kaunti.
Manaibu wa magavana walielendeleza wito wa kutaka kupewa bajeti yao katika masuala ya uongozi.
Walizungumuzia swala hilo kwenye bunge la Seneti kuhusu masuala ya ugatuzi wakiongozwa na mwenyekiti wao Reuben Kamuri.
Manaibu magavana hao waliweza kusema kuwa wana ujuzi na uwezo wa kuweza kutekeleza majukumu mengine ya uongozi katika serikali za kaunti na kuimarisha uongozi mwema.
Waliweza kusema kuwa kwa mara nyingi wamekuwa wakisalia kupangwa na magavana wao bila kupewa majukumu maalum ya kufanya kazi.
Waliweza kusema kuwa wangependa Katiba iweze kubadilishwa ili kuwe na bajeti yao maalum Pamoja na kazi zao ambazo zinatambulikana kikatiba.
Walisema kuwa kwa mara nyingi magavana wamekuwa wakiwatumia kutafuta kura baaada ya hapo wanawatelekeza na kuwawacha katika hali ngumu bila wao kujua hatima yao ya uongozi.
Usemi wa uliweza kuungwa mkono na baadhi ya maseneta kama Mpuri Aburi wa Meru waliosemkuwa kwa hakika manaibau magavana wamekuwa wakipitia hali ngumu katika wakati wao wa uongozi kwa kukosa kazi mwafaka na inayotambulikana kisheria.
‘’Ni wazi kuhusu kile mbacho manaibu wa magavana wanastahili kuwa wakifanya lakini ni jambo la kusikitisha kuona magavana hao wanafanya kazi katika huruma ya Magavana jambo ambalo ni la kusikitisha sana inasitahili sheria zibadilishwe ili tuwe na kazi maalumu na bajeti maalum ya kutekeleza baadhi ya miradi mbalimbali katika serikali za kaunti’’. Ruben Kamuri mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ugatuzi alisema.
‘’ Ninaunga mkono pendekezo hilo la manaibu magavana kupewa bajeti yao ili waweze pia kuendeleza baadhi ya sera za maendeleo katika uongozi wa Kaunti mwanzo hawa viongozi wana ujuzi na tajiriba pana kuhusu uongozi’’ Mpuri Aburi alisema
Kwa mara si moja kumeshuhudiwa mizozo na mwingiliano wa masuala ya uongozi kati ya magavana na manaibu wao kuhusu uongozi jambo ambalo huisha kusababisha kukuwa na miswada ya kung’atua magavana uongozini jambo ambalo huleta vita vya kimaslahi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!