Naibu rais Kithure Kindiki amekutana na mawaziri mbalimbali kujadili ufanikishaji wa maendeleo ya serikali.
Alikutana na mawaziri hao katika makao makuu yake ya Karen Nairobi ili kujadili ufanikishaji wa maendeleo ya serikali mnamo Aprili 11,2025.
'' Kamati za mabaraza huweza kurahihisha na kufanikisha utoaji wa huduma katika kamati za mabaraza kwa kuhakikisha kuwa ajenda,sera, miradi na maendeleo ya serikali inawafikishwa kwa ajili ya wananchi kwa haraka'' Kindiki aliandika katika ukurasa wake wa X.
.Alihitimisha mkutano huo kwa kufanya mazungumzo mapanna kwa kuweza kufanya kikao maalum na wizara ya fedha barabara, wizara ya ardhi nyumba na makao ambapo masuala mengi yanayohusiana na kuimarisha uchumi , kuendeleza kupata masoko mbalimbali ya kifedha na vilevile kuendeleza uongozi bora ni baadhi ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa upana zaidi katika kiao hicho.
Profesa Kithure Kindiki alichukua jukumu hilo ili kuweza kuongoza baraza la mawaziri kama jukumu lake kuu la kikatiba ambalo anastahili kulitekekeza kisheria.
Mawaziri mbalimbali kutoka katika wizara zao huweza kuleta ripoti maalum ya jinsi wizara na idara zao zinavyopiga hatua kimaendeleo ikiwemo changamoto ambazo zinapitia na halikadhalika suala la ukaguzi wa maendeleo na hatua chanya pia huweza kuangaziwa ipasavyo katika kikao hicho cha mawaziri.
Baada ya masuala hayo yote kujadiliwa na kila wizara kutoa maelezo muhimu ya kile ambacho kinahitajika kuwa kinafanyika na hatimaye ripoti ya mwisho kuandikwa ambapo Naibu wa rais huweza kumpekelekea rais ambaye huisoma na kueza kutoa maoni yake kuhusu majadiliano na hali nzima ya baraza.
Katika kikao cha tarehe 11 Aprili, 2025 mawaziri waliohudhuria ni Alice Wahome wa Ardhi nyumba na makao,John Mbadi Waziri wa Fedha,Davis Chirchir wa barabara,James opiyo Wandayi waziri wa Kawi,waziri wa mazingira Deborah Barasa,waziri wa utali Rebecca Miano,Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor,na katibu wa baraza la mawziri Mercy Wanjau pia alikuwepo katika mkutano huo. hii ni kuashiria kuwa mawaziri hawa wanajizatiti kwa kila mmoja kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!