
Waziri wa afya Adeni duale alifanya mkutano na muungano wa makitari nchini KMPDU
Ni mkutano ambao ulifanyika mnamo tarehe 10 Aprili 2025 katika jumba la afya jijini Nairobi.Muungno huo wa madaktari uliweza kuwakilishwa na katibu mkuu wa muungano huo Daktari Davji Bhimji Atellah na mwenyekiti Daktari Abidan Mwachi ana viongozi wengine wa ngazi za juu katika muungano huo.
Wazrir Duale aliweza kuandamana na katibu wake wa kudumu Mary Muthoni ambapo kupitia kwa wizara hiyo ya afya ilijitolea kuhakikisha kuwa inajenga ukuruba na kufanikisha mipango miema na muungano wa madaktari.
Wizara iliweza kuhakikisha kuwa na kusema kuwa ilikuwa imejitolea kwa kuwapongeza matabibu wato kwa kuhakikisha kuwa walikuwa wanafanya kazi kwa kujitolea na kuweza kuleta uhusiano mzuri.
Wizara iliweza kuwapongeza madaktari kwa kuwa mstari wa mbele kwa kuwashughulikia wagonjwa kwa kuwapa matibabu kwa usawa na kwa moyo wa kujitolea.
Hata hivyo wizara iliweza kusema kuwa kutokana na juhudi na bidii ambazo madaktari wamekuwa wakifanya wiza ra ya afya ilikuwa na mpango mwema wa kuhakikisha kuwa inashughulikia matakwa na maslahi yao kwa uzuri kwa kuhakikisha kuwa inaimarisha mifumo ya afya kwa wote alimaaruufu taifa care.
Wizara kupitia kwa Duale ilisema kuwa ilikuwa inashirikiana na washikadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa inawapa madaktari maslahi ambayo yanafaa na vilevile kuweza kuzungumza ili kupata suluhisho ya kudumu kutokana na malimbikizi ya mishahara na mikataba mabalimbali.
Duale pia aliweza kusema kuwa kama wizara walikuwa katika hali ya kuhakikisha kuwa wanajitolea ili kuweza kufanikisha na kutekeleza mikataba yote ambayo imekuwepo kwa muda mwingi na ambayo haijatekelezwa.
Duale alishukuru sana muungano wa madaktari pamoja na viongozi wao kwa kuwa mstari wa mbele na kuonyesha ari ya kushiriki katika midahalo ya upatanishi ambayo inalenga kuhakikisha kuwa pande zote zinatimiza malengo husika kwa uzuri.
Duale alisema kuwa kutokana na hio mipango mipana kwa ushirikiano na madaktari hawa kutakuwa na ufanisi mkubwa katika wizara ya afya na kukuza umoja na kufanikisha mpango wa afya kwa wote alimaarufu UHC kote nchini.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!