caption

Wanafunzi wasiokuwa na hatia walijipata katika hali tete baada ya maafisa polisi kurusha gesi ya kutoa machozi katika shule ya upili ya Kiribon eneo la Rongai Nakuru.

Wanahabari pia hawakusazwa walijipata pabaya Jumatano usiku wakati maafisa wa polisi walipowarushia vitoa machozi kuwatawanya walipkuwa wakifuatilia jaribio la polisi kumzuia aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala kuingia katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Kirobon eneo la Ronagi kaunti ya Nakuru.

Vurumai hizo zilisababishwa na mchezo wa kuigiza wa shule ambao unafaa kuigizwa na shule ya upili ya Wasichana ya Butere "Echoes of War" katika mashindano ya shule za upili yanayoendelea ambao unadaiwa kuandikwa na Malala.

Polisi walilizingira gari la Cleophas Malala - mwandishi wa tamthilia hiyo katika jaribio la kumzuia kuingia katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Kirobon.

Malala aliripotiwa kuwa na nia ya kusimamia mazoezi ya mwisho ya tamthilia hiyo, ambayo iliyokuwa imepangiwa kuigizwa Alhamisi asubuhi katika Shule ya Msingi ya Simba, mojawapo ya maeneo yanayoandaa  Tamasha za Kitaifa za kuigiza kwa shule.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mchezo wa kuigiza ulikataliwa wakati wa Tamasha za Kanda ya Magharibi chini ya hali isiyoeleweka.

Uamuzi uliofuata wa Mahakama Kuu ulibatilisha uamuzi huo, na kurejesha mchezo huo na kuamuru kujumuishwa kiwango cha kitaifa.

Kufuatia agizo la mahakama, wanafunzi ambao tayari walikuwa wameondoka kwa likizo ya Aprili walirejeshwa kuendelea na mazoezi.

Saa tatu usiku Alhamisi, polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandishi wa habari waliokuwa wamepiga kambi nje ya shule hiyo ili kuripoti hali ulivyokuwa.