Seneta wa zamani wa Kakamega na mwandishi wa tamthilia tatanishi ya Echoes of War alilala katika kituo cha polisi cha Eldamaravine.

Akizungumza na  kituo cha Runinga  cha Citizen mnamo tarehe 10 Aprili kupitia kwa njia  ya simu  na mtangazaji  Rashid  Abdala alielezea  wananchi kuhusu hali yake ilivyo.

'' Jana nilikuona  ukiwa  umezuiliwa ili kutoweza kuwasalimia  wanafunzi wako na  kuwajulia hali huku ukiwa  katika  pilikapilika za kuhakikisha kuwa unajianda  kwa hafla  ya siku iliyofuata, sijui  kwa  sasa  uko wapi na  ulilala wapi? Rashid Abdala alimuuliza.

Kwa sasa niko katika  kitu cha polisi cha EldamaRavine hapa ndiko nilikolala kwa sasa hivi  bado nimeshikwa  niko katika kituo cha   polisi,polisi   wamejaa huko nje  na  ilihali wamekatata  kuniambaia makosa  yangu  ni  gani?

 Ninakashifu  hicho  kitendo   vikali kwa  maana  ni  kitendo  ambacho  kinalenga kuwaadhalilisha na  ninalaani kitendo  cha kuweza  kuwaondoa na kuwanyima watoto wetu uhuru wa kujieleza  na kuweza  kuimarisha vipaji vyetu kwa kutumia  talanta. 

Nimekuwa nikiuliza makosa yangu ni gani kuhussu kushikwa huku  kisha ninaambiwa kuwa  ni amri kutoka juu kwa hivyo nigependa kumrai rais  pamoja na uongozi wa serikali kuu kwa jumla ningependa kumwambia rais  kuwa vita vyetu  kama wanasiasa visitumike  kuwaelekezea watoto pia.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Rais ni vipi unakanya  mchezo huo  usichezwe na ilihali haujauona   tena ningependa  kusema kuwa mchezo huu ulianza kupata ushindi katika viwando vya maeneo bunge  na kuweza  kushinda  katika ngazi ya mkoa  na kupata alama 90 kuashiria kuwa ni mchezo wa kuigizwa  ambao una tija sana kwa jamii.

 Ila kwa upande wangu ningependa kusema kuwa tuweke  kando siasa  na kuweza kuhimiza umoja na  utangamano bila kuwajumuisha watoto wadogo ni haki yao kushiriki katika  michezo hii ya kuigizwa'' Malala alisema.

 Alipoulizwa kuhusu kile  ambacho sasa alikuwa ameandikisha  kortini kutokana na  kukamatwa  kwake  alisema kuwa hapakukuwa na andikisho lolote  la makosa  yake  ila  akasema kuwa  mawakili wake wakiongozwa na wakili Ken Echesa  walikuwa wakifanya  kila juhudi kwa  ushirikiano  na afisi  ya mkurugenzi ya mashitaka  ya umma  ODPP ili kuweza  kutegua  kitedawili hicho.

 Wanafunzi wa Butere waliweza kufika katika  jukwaa kisha wakaaimba wimbo wa  taifa  na  hatimaye  wakaondoka  kulingna na video na sauti zilizonaswa.