
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen aliendeleza kampeni yake ya usalama katika eneo la Pwani ya Kenya.
Ni kampeni ambayo aliipa jina la Jukwaa la usalama maeneo ya pwani ya Kenya ambapo ililenga kutoa usalama kwa wakaazi wa eneo hilo na kuondoa makwekwe na vizingiti katika maeneo hayo.
Katika shughuli ya kutupilia mbali zoezi la upigaji msasa wa wananchi kwa ajili ya kupata vitambulisho pia lilijadiliwa katika msururu wa kampeni ya usalama katikla eneo hilo.
Vilevile aliweza kuzungumzia suala la kupata vitambulisho bila kuhitaji kutuma maombni zaidi na kuweza kusubiri kwa muda kama awali huku akisema kuwa hatua hiyo kwa sasa serikali ilikuwawa imechukua hatua madhubuti kwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapokea vitambulisho hivho bila kutatizika akisema kuwa ilikuwa huduma ambayo ilikuwa ikitolewa kwa wananchi wote bila kuzingatia ubaguzi wowote.
Waziri Murkomen pia aliweza kukagua zoezi hilo katika eneo bunge la Mokowe ambapo shughuli ya watu kujisajili kwa ajili ya kupata vitambulisho lilikuwa likiendelea katika kaunti hiyo ya Lamu.
''Tutasikiliza na kuwashirikisha maafisa wa usalama katika vitengo vyote ili kuhakikisha kuwa tunawasikiliza washikadau wote wakiwemo wananchi kuhusiana na matukio ya usalama.
Vilevilee huduma za usalama kwa wananchi pia zitaaweza kutolewa ili wananchi waweze kufaulisha mipango yao kwa kupata huduma zote za serikali kutoka kwa serikali bila ubaguzi wala upendeleo wowote '' Waziri Murkomen aliweza kufafanua,.
Itakumbukwa wazi kuwa waziri Murkomeni amekuwa katika pilikapilika za kuendeleza shughuli za usalama katika sehemu zote za taifa ikiwemo na kujihakikisha kuwa anahamasisha umma ni kwa ajili ya kuwaeleza ili waweze kujisajili na kupata vitambulisho vya kitaifa.
Mwezi jana aliendeleza zoezi hili katika kaunti ya Nakuru huku akiwahiimiza watu kuhakikisgha kuwa wanajisajili ili kupata huduma hiyo muhnimu ya kitambulisho.
Katika Kaunti ya Lamu aliweza kuandamana na viongozi kama Gavana Issa Timamy seneta Joseph Gichuki, mbunge Obo Ruweida Lamu mashariki, Stanley Muthama wa Lamu magharibi na naibu inspekta mkuu wa polisi Gilbert Masengeli.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!