Mbunge wa Nyando Mheshimiwa Jared OKello alisema kuwa Cleophas Malala alikuwa anatafuta huruma kutoka kwa umma.

 Alikuwa akizungumza katika mahojiano na  runinga moja nchini mnamo tarehe 10 Aprili ,2025 ambapo alisema kuwa  juhudi za aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala alikuwa anajitafutia sifa kutoka kwa wananchi.

'' Ceophas Malala si mwandishi wa vitabu wala mwandishi wa mashairi kwa vyovyote vile kwa  hivyo kusema kuwa alikuwa anapanga kuzindua kitabu cha tamthilia cha Echoes of War hiyo ilikuwa ni njia mojawapo ya kutaka kujipalia  sifa  na huruma kutoka kwa wananchi. 

 Malala kwanza alitaka kujinadi na kuonyesha umma kuwa alikuwa akitendewa unyama hata unapotazama katika video ambayo tuliona  siku ya tarehe 9 Aprili , 2025 usiku saa tatu utajiuliza  ni kwa nini alikuwa mahali pale wakati  huo?

Tena aliweza  kusababisha hali ya sintofahamu  kwa kuweza kuwavutia watu wengi kuashiria  kuwa alikuwa na nia fiche  ya kuonyesha  umma  kuwa  alikuwa akifanyiwa matendo mabaya ilihali si hivyo. 

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 Hata  unapotazama kulikuwepo na  maafisa  wa polisi ndio lakini aliweza  kujinadi na kujitanua ili  kuonyesha serikali kuwa ilikuwa  katika upande  mbaya wa  kumshika bila makosa  hata  aliweza kusababisha baadhi ya wanahabari kutoka idhaa mbalimbali  kama Maryann Nyambura  waliokuwa wakitekeleza wajibu wao kisheria kupigwa  na  vitoza machozi hadi kuumia  bure'' Okello alisema.

 Kwa  upande mwingine Malala  alikuwa  pale kaunti ya Nakuru ambapo michezo ya Drama kiwango  cha kitaifa  iliuwa yafaa kuigizwa.

''Mbona mnataka kunishika je, nimetekeleza kosa  lipi?Mbona mnishike bila makosa yoyote?''

Malala  aliuliza maswali mengi  kwa mkuu wa  kiengo cha DCI eneo la Nakuru alikuwa na msururu  wa maswali mengi huku  kando yao kulingana na video iliyowanasa kukiwa na maafisa wengi wa  polisi wakiwa wamesimama kando yao.

Malala alikuwa ameandika Tamthilia kwa jina Echoes  of war tamthilia ambayo ilikusudiwa  kuigizwa na  wanafunzi wa  shule  ya upili ya wasichana ya Butere. 

 Kulingana na  duru za  kuaminika ni kuwa tamthilia hiyo ilikuwa na maudhui ambayo yalikuwa yanalenga kuikosoa na  kuchambua masuala mengi ambayo yalikuwa yamejikita katika mambo ya  uongozi na utawala. 

 Kutokana na hilo serikali iliazimia  kusimamisha  uigizaji wa  drama hiyo na vilevile kuwazuia wanahabari kuweza kunasa picha na video za wanafunzi hao wakiigiza.

Inasemekana kuwa  uongozi wa shule hiyo kupitia kwa  mwalimu mkuu uliazimia kufutilia mbali uigizaji wa tamthilia  hiyo kutokana na hali tete ambayo imeibuka na vita vya kimasilahi kati ya serikali na  shule  hiyo.