Duale aongoza katika utiaji sahihi wa mikataba ya utendakazi

Waziri wa afya Aden Duale allihudhuria shughuli ya  kutiwa sahihi kwa mkataba wa utendakazi wa fedha wa mwaka 2024/2025.

 Mikataba hiyo ya utendakazi ilifanyika na mashirika ya kiserikali ya Semi Autonomous  government na bodi za udhibiti katika izara ya afya.

Katika wizara hizo Duale alisisitiza umuhimu wa mikataba ya utendakazi katika idara za serikali akisema kuwa huweza kusaidia kuweka rekodi ambayo imenyooka ambayo huwa imelingana na hitaji la  sera za kitaifa.

Alisema kuwa hiyo mikakati  hueza  kufanikisha uajibikaji na huhimiza mazoea ya kuweza kutekeleza nakudumisha matukio  kwa wizara nzima katka idara na afisi za mawakala.

''Tupo katika wakati wa muhimu sana katika idara ya afya, Matarajio kutoka kwa  mheshimiwa Rais na wananchi wa Kenya yako juu sana hasahasa katika mpango mzima wa kutekeleza bima ya matibabu ya SHI katika mfumo  wa taifa care.'' Duale  alisema haya akirai mashirika hayo kwa kusema kuwa ni lazima yajitahidi  ili kupunguza makosa ya moja kwa moja.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alisema kuwa mikataba  ya mwaka huu ililenga  kuhakikisha kuwa inaimarisha mpango wa SHI ambao kwa kufanya hivyo  unatekelezwa pamoja na programu ambazo ni muhimu ili kufanikisha mpango maalumu wa huduma za afya kwa  wote alimaarufu UHC.

Duale alizidi kusisitiza kwa  kusema kuwa uhitaji wa mpango huo kwa kuimarisha viwango vya afya katika viwango vya kitaifa  alieleza na kusisitiza kuhusu  SAGA  ili kuhakikisha kuwa wizara inaimarika zaidi na inaongeza utendakazi wake ili kupunguza visa vya ufisadi ndani ya wizara.

Utiaji sahihi  wa mipango hio ilieza kuakisi mkataba mwingine ambao Rais alikuwa ameutia sahihi na  mawaziri wa afya waliotangulia kwa  ushirikiano na makatibu wa kudumu wa afya.

Lakini mpango huo uliweza kucheleweshwa kutokana  na ukaguzi na udhibitishaji  wa  stakabadhi husika  ingawaje aliweza kusema kuwa baadhi ya mashirika yalikua tayari yameanza  utekelezaji huo kuashiria ile  hali ya kujitolea kisawasaswa katika kufanikisha  mpango huo.

 Waziri aliweza kuwarai viongozi wa mashirika mbalimbali kuweza kujiwekea viwango vya utendakazi katika mashirika yao  na akasisitiza kuwa wafanyakazi wataweza kupigwa msasa kutokana na matokeo ya rekodi ya utendakazi  kwa kuangazia mambo kama heshima, maadili,ushirikiano na matumizi mazuri ya maliasili.

Duale alikua pamoja na katibu wa kudumu katika wizara  ya afya Mary Muthoni, afisa wa afya katika hospitali za umma Harry Kimtai  pamoja na mkurugenzi wa afya Daktari Patrick Amoth.