Richard Onyonka Seneta wa Kisii

Seneta wa Kisii Richard Onyonka amesema kuwa serikali za kaunti hazifanyi vyema kama ilivyotarajiwa.

 Kulingana na usemi wake  Onyonka alisema  kuwa kulingana na matumaini mengi yaliokuwa katika wakaazi pamoja na wananchi wengi walikuwa na matarajio mengi kuwa Serikali za kaunti zingerahihishia wananchi huduma.

Onyonka  alisema kuwa baada ya serikali hizo kugatuliwa na kupewa majukumu mbalimbali ya  kutekeleza halikadhalika   kuwa na bajeti yake rasmi bado kuna matatizo mengi  yanayozikumba.

''Serikali zetu za Kaunti bado zina safari ngumu ya kutekeleza pamoja kuhakikisha kuwa zinajikwamua kutoka kwa mitego ya madeni na utumizi mbaya wa pesa za umma ili kuhakikisha kuwa miradi na maendeleo inapatikana kwa wananchi bila mizozo wala mikwamo ya mara kwa mara.

Katika viwango tulivyofikia kwa sasa Kaunti hazifanyi vizuri na tulikuwa tunatarajia kuwa kufikia sasa maendeleo katika ngazi ya  Kaunti yangekuwa yameshamiri na kuleta mwamko mpya kwa raia jinsi ambavyo watu  walikuwa na matumaini makubwa ya katiba yetu pamoja na  serikali  za Kaunti.'' Onyoka alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika serikali za kaunti kuna masuala mengi ambayo yaligatuliwa kama afya, ujenzi wa barabara, maji na masoko mambo ambayo yalikuwa yakitekelezwa na serikali kuu.

Hata hivyo  baada ya hayo yote bado kuna matatizo mengi ambayo yanasumbua usimamizi na udhibiti imara wa serikali hizo.Mgao wa bajeti kutoka kwa serikali kuu uliweza kucheleweshwa kwa mwezi wa Pili na tatu wa mwaka wa 2025-2026.

Mwenyekiti  wa kamati ya bajeti wa baraza la magavana nchini bwana  Fernandes Barasa aliweza kusema kuwa Baraza hilo lilikuwa na nakisi ya upungufu wa ahilingi bilioni 63 pesa  ambazo kaunti zilikuwa   zinadaiwa ili kuhakikisha kuwa zinatekeleza mipango yake na kuendeleza usimamizi wake vyema.

Wakati huo huo mambo hayo yanaposhughulikiwa ya utepetevu  wa serikali za  kauntti  kuna mzozo wa uongozi ambao ulichipuka katika kaunti ya Nyamira ambapo  mabunge mawili ya wawakilishi wadi yaliweza kutengenezwa na kuweza kutangaza misimamo yake kuwa kila bunge lilikuwa halali kisheria.

 Mabunge hayo yamekuwwa yakisisitiza kupata mgao wa bajeti kutoka kwa afisi ya mdhibiti wa  bajeti ya serikali  ili kila moja iweze kuendeshashughuli zake za serikali.

Mizozo miongoni mwa Magavana pamoja na wawakilishi wadi imekuwa ikishamiri na kusababisha baadhi ya Magavana Kutimuliwa ofisini. 

Kwa  sasa kinachosubiriwa kuhusu hatima ya Kaunti ya Nyamira ni kuona ikiwa bunge la  Seneti litaweza kuangazia hoja ya kuweza kujadili kuvunjiliwa mbali kwa gatuzi hilo kupitia kwa maamuzi ya rais.