
JUKWAA la Songa Play ndio Habari mpya ya mjini linapokuja suala la burudani isiyokata na ambayo inakuja kwako wakati wowote bila malipo.
Songa Play, jukwaa ambalo lilizunduliwa Agosti 2024 na kampuni ya Radio Africa Group, limetajwa kuwa miongoni mwa majukwaa machache ambayo yameleta athari kubwa na Chanya katika tasnia ya burudani inayokua kwa kasi ya umeme.
Jukwaa hilo sasa linapatikana si tu kwenye watumizi wa vifaa vya Android, lakini pia kwa wapenzi wa vifaa vya IOS, msiseme zaidi, kwani Songa Play ipo viganjani mwenu.
Ili kuipata Songa Play na kufurahia vipindi vyako pendwa vya stesheni zote za Radio Africa, podikasti, mfululizo wa miziki ya kila aina na burudani nyingine, fuata hatua hizi nyepesi;
1. Google PlayStore ama AppStore
Kwa watumizi wa vifaa vya Android, elekea kwenye programu ya Google PlayStore na wale wa vifaa vya IOS, fungua programu ya AppStore.
2. Tafuta ‘Songa Play’
Baada ya kufungua, utakaribishwa kwenye programu hiyo na juu kabisa kuna alama ya ‘Search’. Bonyeza hicho kitufe kisha uandike ‘Songa Play’.
Bila ubishi wowote, utaletewa programu ya Songa Play ambayo ina rangi nyekundu kwenye nembo yake yenye muundo wa ‘S’.
3. Pakua
Baada ya kuibonyeza nembo hiyo ya Songa Play, itakuletea maelezo zaidi, la kwanza ikikuuliza iwapo ungetaka kuipakuwa kwa kimombo ‘Install’.
Ukiteremka chini kwenye kiwambo chako utaona maelezo kuhusu programu ya Songa Play, maoni ya watu na idadi ya watumizi wake.
Ukibonyeza ‘Install’ programu ya Songa Play itapakuliwa moja kwa moja kwenye kifaa chako bila malipo yoyote, lako tu ni kuwa na unganisho kwa huduma ya intaneti pekee.
4. Fungua
Ili kujua kama programu ya Songa Play imemaliza mchakato wa kupakua, kitufe cha ‘Install’ kitageuka na kuwa ‘Fungua’.
Bofya kwenye hicho kutufe cha ‘Fungua’ na moja kwa moja utakuwa umeingia ndani ya Songa Play.
5. Jisajili
Baada ya kuingia kwenye Songa Play, utakaribishwa kisha utatakiwa kutoa maelezo yako ya kujisajili – huduma ambayo ni ya bila malipo.
Baada ya kujisajili kwa kutumia maelezo yako ya barua pepe, Utaona kichupo cha kukutaka ufanye uamuzi kama unaanza kusikiliza, na ishara ya mshale unaoelekea upande wa kulia.
Fuata huo mshale kwa kuubofya kisha chaguoa burudani unayotaka kuisikiliza kutoka miongoni mwa safu ya huduma nyingi kutoka podkasti, nyimbo na vipindi vya Radio zote za shirika la Radio Africa Group.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!