ISAAC MWAURA , Msemaji wa serikali

Msemaji wa  serikali Isaac Mwaura amesema kuwa hakutakuwa na mswada wa fedha wa mwaka 2025.

Mwaura aliweza kukashifu na kusema kuwa mwaka huu hakutakuwa na mswada  wa  fedha wa mwaka 2025  alisema kuwa mwanzo wanasubiri bajeti itoke katika bunge  la taifa  mwisho wa mwezi huu ili waweze kuangazia makadiria ya bajeti ya shilingi trilioni 4.2.

''Ningependa kusema kwa kusisitiza kuwa mwaka huu hakutawa na mswada wa fedha mwaka 2025  tunasubiri makadirio ya majeti yatoke kwenyue bunge mwishoni mwa mwezi huu.

 Ila  kuna baadhi ya watu ambao wameanza kusambaza habari za uongo  hizo katika mitandao wakisema kuwa  serikali inapanga kutoza wananchi ushuru mwingi hao  ningependa kuwatangazia kuwa hao ni maaadui wa nchi wasiotutakia mema  na wanatumia mitandao ya kijamii ili kuweza kuchochea umma  ambapo  si  vyema''. Mwaura alifafanua.

Kuhusu maswala  ya usalama ambapo  jengo  la gorofa  linatarajiwa kubomolewa kule  sehemu  za Mombasa Msemaji wa serikali aliweza kusisitiza akisema  kuwa hiyo ilikuwa chini ya sheria na katiba  ya Kenya kuwa  iwapo kunapotokea swala la janga la usalama  wa  kitaifa  hivyo  huhijtaji  sana kwa haraka usimamizi  wa jeshi la nchi ili kuhakikisha  kuwa  kila kitu kinaenda sambamba.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Upange wa kilimo hasahasa upande wa ugavi  na usambazaji wa mbolea  kwa  wakulima alisema kuwa hamna mpango wala notisi kwa kusema kuwa mbolea ambayo inatolewa na serikali inauziwa kwa gharama alieza kusema kuwa mpango huo  wa mbolea ya ruzuku una  utaratibu maalum   serikali  ilikuwa ikishirikiana na serikali za Kaunti ili kuhakikisha kuwa kilakitu  kinakwenda sambamba.

Kuhusu  suala la chama  cha wakulima kuweza  kusema kuwa wanajipanga kuweza   kujiondoa  katika serikali ya kenya kwanza msemaji  alidokeza kwa kufafanua  kwa  kusema kuwa  serikali ilikuwa  ikidumisha uhusiano mwema  kati ya  wakulima  na serikaili . 

Alisema kuwa wakulima wa miwa waliweza kupokea bonus jambo ambalo ni la kujivunia  ambapo  alisema kenya ina jumla ya kampuni 16 ambapo 4  kati  yazo zinamilikiwa na serikali  na  kama njia mojawapo  kwa kuimarisha hali zao vyema serikali imeimarisha sekta hiyo ya kilimo.

Alisema kuwa Kenya ilikuwa ikisafirisha na kuuza zao la majani chai kwa mataifa ya nje kwa kiwango  kikubwa  akisema kuwa  Kenya ilikuwa inafanya vyema katika soko la limataifa kwa viwango  vyote vya mazao.