Waziri wa afya

Wizara ya Afya imetangaza mkurupuko wa ugonjwa  wa kipindundu nchini

Ni tangazo ambalo lilitolewa mnamo Aprili 8, 2025  na wizara ya afya ambapo ilisemekana kuwa  msambao huo wa maradhi ya kipindupindu yaliathiri sehemu mbalimbali za  taifa.

Kipindupindu ni ugonjwa hatari ambao maambukizi yake  hutokana na viini ndani ya maji vinayosababishwa na kiini kiitwacho VIBRO CHOLERA , ambapo ugonjwa huo husababishwa na mtu kula chakula kichafu ambacho kina kiini.

Dalili za maradhi haya ni kutapika , kuumwa na misuli na kupoteza maji mwilini kwa wingi  ambapo hudumu kwa muda wa saa mbili na  tatu.

Kulingana na  taarifa ya hali ya afya imedokeza kuwa kuanzia tarehe sita Aprili ,2025 jumla ya kesi 97 ikiwemo vifo vya watu sita vilikua vimeripotiwa ambapo ni kiwango cha asilimia 6.2 ambapo kesi hizo zliliripotiwa maeneo ya Migori ,Kisumu,na Nairobi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika kaunti ya Migotri kesi 53 ziliripotia kikwiemo kifo  cha mtu mmoja na maeneo yalioathirika ni Suna magharibi, Suna mashariki,Kuria magaribi na Kuria  mashariki.

Katika kaunti ya Kisumu kesi 32 ziliweza kuripotiawa   ambapo kesi 4 za vifo ziliripotiwa  na maeneo yalioathirika ni Nyando na Muhoroni.

 Katika kaunti ya  Nairobi kesi 12 ziliripotia kisha mtu mmoja  aliweza kuaga dunia  na  maeneo yaliyoathirika ni  Kasarami ,Embakasii  mashariki, embakasi ya kati Roysambu,Kibra na Dagorreti Kusini .

 Wizara ya afya inashirikiana na serikali za kaunti  ili kuhakikisha kuwa  inazuia msambao wa maradhi hayo.

Wizara imeanzisha mikakati ya kuhakikisha kuwa inafanya ukaguzi wa karibu  sana ili kuweza kuhakikisha kuwa hamna kesi nyingi zinazoripotiwa.

Kuwapa mafunzo mafisa wa afya  kwa ushikiano na maafisa wa utabibu, inawapa madktari mafunzo maalumu ya  jinsi ya kukabiliana na maradhi hayo hatari.

Kwa kuhakikisha kuwa inasambaza habari kwa kutumia waendelezaji wa huduma za  afya mashinani pamoja na kutumia vyombo vya habari kuweza  kujiendeleza na kuzuia msambao 

Umma kwa upande mwingine umeombwa kuhakikisha  kuwa wanapata huduma za matibabu kwa haraka na kuhakikisha kuwa wanadumisha viwango vya usafi vya hali ya juu kwa mfano kwanzia kwa kiwango cha mtu binafsi hadi kwa jamii kwa jumla.

 Kunywa maji safi na kula chakula ambacho pia  ni safi na kupata matibabu ya upesi  iwapo dalili hizo zitaendelela.