Gavana Abdulswamad Nassir Mombasa 

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir alitangaza utaratibu wa kubomoa ghorofa kwa njia ya kutumia kilipuzi.

Alipoitisha kikao na waandishi wa habari sikui ya Jumanne 8 Aprili,2025   ili kuweza kuelezea utaratibu wa mpango huo utakaoendeshwa na jeshi.

Gavana aliweza kusema hayo akiwaleta pamoja viongozi wa ngazi za mitaani pamoja na machifu ambao walipewa agizo la kuhakikisha kuwa utaratibu wa kuwaondoa katika gorofa hiyo unafanikishwa kwa wepesi.

 Aliweza kuwaagiza wananchi mbalimbali kuwa wanastahili kusonga umbali wa kilomita moja  na mita mia mbili ili kujihakikishia usalama wao wa afya .

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 Ubomozi huo unalenga mijengo yote  ambayo haijajengwa sawa na kusema kuwa majengo hayo yataweza kubomolewa na wanajeshi ambao kulingana na maelezo ya Gavana watakuwa wamejisitiri vyema kutokanana  athari ya mlipuko wa sauti na vilevile kujikinga na vumbi itayosushudiwa wakati wa ubomozi huo.

''Mahali tulipofika hamna vile tutazidi kutulia itabidi kuhakikisha kuwa ubomozi huo lazima utekelezwe kwa utaratibu wa hali,, kwa hivyo watu ambao wanakaa karibu na tukio hili itabidi mhame na mwende mbali kidogo , kesho asubuhi mnapoamuka hakikisheni kuwa mnasonga kwa umbali wa kilomita 1 na mita mia mbili.

Kesho kwanzia saa kumi na moja asubuhi mtu yeyote asiende karibu na mahali ambapo shughuli hiyo itakua ikifanyika watu  wasiende katika madarasa , wala shule za mtaa huo hazitafunguliwa kesho, hio ni kwa ajili ya manufaa ya usalama wao.

Sehemu zitakazo athirika ni mtaa wa bakistani na Marikiti hivyo jumba likianguka kuna uwezekano kuwa vyuma na mawe ambayo yanayoweza kuleta shida'' Gavana alisema. 

Aliwarai wakaazi wa eneo hilo kuwa makini  na kuwa wangalifu wakati wa tujio hilo adhimu ili kuepuka hasara  yoyote ile itakayotokea.

Gavana Abduliswamadi aliweza  kuwaelezea wakaazi hao wa Mombasa ili waweze kuzingatia utaratibu huo kwa makini na kwa  uzalendo wa kipekee.

Alieza kuwambia  kuwa katika hospitali kuu ya rufaa  ya Mombasa waliweza kuhamiswa kutoka katika vitanda vya wagonjwa mahututi huku akiawambia kuwa wajaribu kuwa wenye kuzingatia umuhimu wa maisha  yao kwa kutojiwasilisha  mahali ambapo tukio hilo litakuwa likitendeka.