Kiongozi wa Third Way Alliance Ekuro Aukot

Kiongozi  wa chama cha TWA Third Way Alliance Ekuru Aukot amesema kuwa kiongozi ambaye amekuwa  uongozini  kwa muda  mrefu nchini ni Rais William Ruto.

Aukot alikuwa akizungumza katika mdahalo mzima wa hali halisi ya taifa katika idhaa ya Runinga ya Citizen  mnamo Jumanne Aprili 8,2025 wakati alipotoa hoja  hiyo kwa  kusema kuwa rais Ruto ndiye  kiongozi ambaye amekuwa kwenye madaraka  ya uongozi kwa muda wa miaka 28 sasa.

Aukot alidokeza hayo akisema kuwa Tangu Ruto achaguliwe mnamo mwaka wa 1997 kama mbunge wa Eldoret Kasikazini  amekuwa katika nafasi za uongozi kutoka idara moja hadi nyingine hadi kufikia leo.

Ila licha ya kuwa  katika uongozi kwa kipindi cha muda mrefu  Aukot alimshutumu kwa  kusema kuwa  hajakuwa akitumia nafasi yake vyema katika uongozi kuweza kusaidia raia ili waweze kujiendeleza na wao.

Aukoti  alimkashifu Rais Ruto kwa kusema kuwa sifa na umaarufu ambao amekuwa akijizolea kila wakati na kupata heshima kuu hamna chochote cha  kujivunia kutoka  kwa raia na baadala yake Ruto amekuwa akijihusiaha  tu  na sifa za kutaka kupata utajiri.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

''Ruto ndiye kiongozi ambaye amewahi kuwa kwenye safu ya uongozi kwa muda wa miaka mingi yule  ambaye  yuko hai baada ya marehemu rais wa Zamani Mwai Kibaki  lakini licha ya hayo yote  hamna chochote  chenye ametekeleza kwa huo muda wake wote ambacho umma utajivunia'' Ekuru Aukot alisema.

''baadala ya kuchukua fursa hiyo ya kuwa na rekodi nzuri ya uongozi kuweza kufanya mambo ambayo yanashabihiana na rekodi yake mamlakani yeye amekuwa tu mstari wa mbele kutaka kujilimbikizia utajiri  ili awe  miongoni mwa wale mabwenyeye katika taifa'' Aukot alizidi  kuelezea.

Aukur Aukot ni wakili na vilevile ni mmoja wa wasisi waliokuwa katika jopo lililoandika katiba yetu  ya kenya ya mwaka wa 2010 na vilevile yeye ni kiongozi wa chama cha Third way alliance.

Ekuru Aukot aliwahi shiriki katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 kama mwaniaji wa urais kupitia kwa tiketi ya chama chicho hicho chake cha Third Way alliance .