
Wizara ya usalama wa ndani kupitia kwa idara ya magereza mnamo Aprili 7, 2025 ilitoa tangazo rasmi katika gareti la taifa kuhusu nafasi za kuwaajiri maafisa wa kuhudumu katika magereza.
Tangazo hilo linawafahamisha umma kuwa kutakuwa na zoezi la kuwajiri polisi wa kuhudumu katika madereza ya taifa mnano tarehe 30 Aprili, 2025 na kutiwa saini na kamishina mkuu wa magereza Bwana Patrick Aranduh
Hitaji rasmi kwa kila atakayetuma ombi la nafasi hiyo ya ajira ni kuwa ni lazima awe na stakabadhi zifuaatazo.
Lazima muomba nafasi awe ni Mkenya na awe na kitambulisho cha taifa vilevile asiwe amehusishwa na kesi zozote za uhalifu.
Ni lazima awe amehitimu masomo ya sekondari akiwa na alama ya gredi ya D+ kuenda juu,awe mwenye umri wa miaka 18 hadi 28, awe na kimo au urefu wa fiti 5 na inchi 4 kwa wanaume ilihali fiti 5 na inchi 2 kwa kinadada.
Vilele mwenye kutuma ombi la kazi ni lazima awe mzima kiafya , viungo vyake vya mwili viwe sawa na awe na akili timamu ni lazima wenye kutuma ombi hili wawe na uwezo mzuri wa kuona na kusikia vizuri.
Hatimaye kwa akina dada hawastahili kuwa na ujauzito wakati wa kuchuliwa au baada na wakati wa kipindi cha mazoezi.
Kwa wale mbao watakaochukuliwa watapitia kipindi cha mazoezi ya kijeshi kwa muda wa miezi isiyopungua tisa.
Zoezi hilo litakuwa ni la bure hamna chochote kitakacho hitajika wala kutumika kama hongo mtu yeyete atakayepatikana akiwa ametumia stakabadhi za masomo ambazo ni ghushi hatachuliwa na badala yake ataweza kushitakiwa kulingana na mijibu wa sheria na kufikishwa mahakamani kujibu mshitaka.
Waomba nafasi hizo watahitajika kubeba kitambulisho halisi cha taifa, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule, namba ya cheti kutoka kwa huduma ya ukusanyaji ushuru KRA PIN.
Wito ulitolewa kwa umma kuwa uangalifu ili kuepuka kutapeliwa na zoezi hilo litafanyika katika sehemu mbalimbali za taifa zilizotajwa.
Mombasa zoezi hilo litafanyika katika gatuzi dogo la Likoni,Mombasa,Nyali,Kisauni,Changamwe na Jovmvu.
Kwale zoezi litaendeshwa katika gatuzi dogo la Matuga,Kinango,Lungalunga,Msambweni Simbahills,Samburu miongoni mwa kaunti zingine kama Kilifi,Tanariver,Lamu,Garissa,Wajir na Mandera.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!