Seneta wa Busia

Seneta wa Busia na ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu Okiya Omtatah alidai kwa  kinywa kipana kuwa Kenya  ni tajiri kupindua  kulingana na mgao wake  wa bajeti.

Kulingana na maelezo ya  bwana Okiya alisema kuwa kulingana na bajeti ambayo Kenya ilijitengea ni bajeti ya  kiwango  kikubwa ambacho  kulingana na yeye kilikuwa kiwango ambacho kilikuwa  kina mgao mkubwa  sana.

Bwana  Okiya  Omtatah aliweza  kusema kuwa  wakati wa kipindi cha aliyekuwa  rais  Uhuru  Kenyatta kulingana na ukaguzi wa hesabu za  rasilimali ya  taifa  Kenya ilikuwa  na shilingi bilioni 900 ambazo zilikuwa zimesimamia  raslimali ya taifa kulingana na benki kuu ya Kenya CBK.

Bwana  Omtatah  alikuwa amefika Kortini kushitaki uamuzi wa aliyekuwa waziri wa fedha enzi zile Akuru Yatan kwa kuondoa msamaha (waiver) kwa shilingi bilioni 900  Korti iliweza kukubaliana na yeye kuwa Serikali iliostahili kurudishia mwananchi mlipa ushuru hela ambazo ilikuwa imejiondolea kama ulipaji ushuru.

Kulingana na maelezo ya  bwana Omtatah alikuwa ameishitaki serikali kupitia benki kuu  kwa kuondoa msamaha wa kulipia  ushuru  kwa shilingi bilioni 900.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Bwana Okiya aliweza kusema kuwa kulingana na tukio hilo ambalo Aliyekuwa waziri wa fedha  Akuru Yatan katika utawala  wa aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta waliweza kuondoa msamaha huo wa  kulipa pesa kutoka  kwa benki kuu ya Afrika(Commercial  Bank of Africa).

 Hata  hivyo kulingana na  matamshi  ya  Okiya  Omtatah, aliweza kusema kuwa kiwango cha bajeti ambacho taifa la  Kenya  lilikuwa nacho  kilikuwa  kiwango kikubwa  cha  mgao wa  bajeti ambacho  hata ukiweka ujumuishaji wa  mataifa ya jumuiya  ya  Afrika Mashariki yote Tanzania,Uganda,Rwanda na Burundi  bado taifa  la Kenya lina raslimali nyingi.

''Kulingana na kiwango cha mgao wa bajeti ambacho taifa la Kenya linalo kulinga na zile pesa ambazo ziko katika maliasili pekee ni shilingi bilioni 900 kiwango ambacho ni cha juu sana chenye  utajiri ''  Okiya alisema.

Alikuwa akizungumza  katika kituo cha Spice fm alipokuwa akidadavua na kuelezea hizo takwimu zake za fedha. 

Hata hivyo baaada ya kushinda kesi aliyokuwa ameiwasilisha kortini siku ya  ijumaa na korti kuamuru kuwa  kwa  shilingi billioni 700  ambazo hazikukuwa zimelipiwwa ushuru juu kwa  kuondolewa zilipaswa kulipwa  kwa  kuwa  ni mali ya mlipa ushuru.