
Jaji mkuu Martha Koome amesisiitiza na kutangaza hatua mathubuti za kupambana na ufisadi katika mahakama zote nchini.
Akitoa hutoba yake ya kuangazia masuala ya mahakama na hali halisi ya huduma za mahakama, Koome alisisitiza kuwa hamna ufisadi katika mahakama na kusema kuwa wazo kama hilo halikukuwepo miongoni mwa wafanyakazi wa mahakama wote.
''Ninataka kuangazia na kuzamia katika suala la maadili na ufisadi katika mahakama zetu chini ya huduma ya kupambana na maadili na ufisadi EACC ambapo kuna madai mengi sana ya ufisadi katika mahakama zetu.,'Koome alisema.
''Hizi ni tetesi ambazo hatuwezi kupuuza ni madai makubwa ambayo lazima tuangazie na tuchunguze ifaavyo.''Koome alisisitiza.
''Ningependa kutangaza na kusisitiza wazi kuwa mahakama ni mahali ambapo hamna ufisadi wowote, jinsi tujuavyo na jinsi ambavyo tunafahamu na tumelizungumzia hili katika mihadhara mbalimbali ni kuwa tunajua sera ya angamiza ufisadi kwa viwango vyote katika mahakama zetu bila kuogopa wala kupendelea ili kuimarisha asasi zetu za mahakama katika viwango vyote tumezindua na kuanzisha kamati mabalimbali katika mahakama zetu kote nchini.'' Koome alifafanua.
'' Hizi Kamati zitakuwa na wajibu wa kuaangazia jinsi majaji wanavyotekeleza kazi zao, kutoka kwa maawakili, waawakilishi kutoka tume huru za kupambana na ufisadi EACC miongoni mwa washikadau wengine.
NI vyema zaidi kama majaji kuhakiksha jinsi majaji wanavyojitahidi kuhakikisha kuwa wanaendasambamba na mifumo ya kisasa ya teknolojia ambapo tumeiona jinsi teknolojia imefanya kazi ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sambamba.
Vileile tuliona jinsi mahakama imekuwa ikitekeleza mambo yake kwa uzuri mwanzo kwa kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda sambamba ikikumbukwa jinsi utumizi wa mitandao ulivyofanya kazi nzuri wakati wa Covid 19''Koome alielezea.
Koome alitoa tangazo hilo la kuhakikisha kuwa anapambana na ufisadi huo na kutoa tetesi nyingi ambazo zimekuwepo kutoka kwa umma pamoja na mawakili waliosema kuwa ufisadi ulikuwa umekithiri katika asasi za mahakama ambapo kupata haki ilikuwa ni vigumu.
Mwezi uliopita rais wa mawakili nchini LSK Faith Odhiambo aliweza kulalamika na kutaka jaji mkuu Martha koome kuangazia hali ya ufisadi katika mahakama zetu nchini.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!