Sarah Mtalii, MD wa Bonfire Adventures//FACEBOOK

MD wa Bonfire Adventures, Sarah Mtalii amewashauri wanawake kuwa na mazoea ya kuchukua likizo fupi katika ndoa wakati matatizo yanapoibuka badala ya kuzivunja kabisa.


Akizungumza kwenye Art of Living ya KTN, Mtalii alisema kwamba matatizo ni kawaida katika ndoa akiyafananisha kama mvua ambayo hunyesha kila mahali.


Aliwashauri wanawake kutovunja ndoa pindi matatizo hayo yanapotokea kwani kuondoka kabisa ni sawa na kutoroka sehemu kunakonyesha ukitarajiwa utatorokea sehemu hakuna mvua – kumbe mvua iko kila mahali.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Hata hivyo, alisema kwamba ni vizuri kwa wanawake kutafuta ushauri nasaha kuhusu ndoa hata kama wanaona ndoa zao ziko katika mkondo salama na pia kushauri kuwa kuvunja ndoa kabisa kunafaa kuja wakati imeshindikana kustahimili manyanyaso.


“Ili kuwa mkweli, bado namaanisha maneno yangu [kwamba mwanamke hafai kuacha ndoa yake eti kisa mumewe ana’cheat]. Kuna kucheat nak una kuchepuka. Hii ya mwanamume kuwayawaya mjini ni suala moja lakini pia kuna masuala makubwa ambayo yanaweza kufanya uondoke katika ndoa yako,” Sarah alieleza.


“Lakini hivyo simaanishi kwamba ukae katika ndoa ambapo kuna cheating, ninachomaanisha ni kwamba ndoa ni Taasisi hakika pengine kama maisha yako katika hatari kubwa. Kuna baadhi ya masuala ambayo yanaweza suluhishwa kwenye ndoa.”


“Wakati mwingine huwa hata napendekeza likizo fupi lakini si kuondoka kabisa katika ndoa. Ndio maana mtu unastahili kutafuta ushauri nasaha, kuna masuala mazito ambayo utaambiwa kimbi lakini pia kuna mengine ambayo unahitaji tu kuchanuliwa.”


“Kama ambavyo tunasema, kunanyesha kila mahali, lakini inapokuja sasa ni mvua ya radi hapo ndipo sasa utaambiwa kimbia,” Sarah alifafanua.


Maelezo yake yalikuwa yakirejelwa ushauri wake wenye ukakasi ambao aliutoa mwaka jana ambao ulipokelewa kwa mikondo tofauti.


Katika ushauri huo, Sarah aliwashauri wanawake kwamba suala la mwanamume kutoka nje ya ndoa kimapenzi si la msingi kusababisha ndoa kuvunjika.


“Ningependa tu kuwadokezea wanawake kwamba haya mambo hutokea. Kila wakati ninapata content yenye naweza chanua wanawake, huwa muda wote naipakuwa kwao.”

“Siku hizi mimi huwaambia wanawake, kwa kweli kuchepuka hakufai kuwa moja ya sababu yetu kuwaacha wanaume au kuanza kuwa na wasiwasi kuhusu wanaume wetu. Hebu acha tuwe na mashaka kuhusu vitu vingine vikubwa kuliko kuwa na mashaka iwapo anachepuka au la,” Sarah alisema wakati huo.