
TUKIO la kushangaza lililorekodiwa kwenye ukumbi wa mazoezi mwanamume akianguka na kuzimia alipokuwa akijaribu kuinua uzito wa kilo 227, limewashangaza watu katika mitandao ya kijamii.
Katika picha hiyo, mwanamume huyo anaonekana akiinua uzani huo mzito, lakini muda mfupi baadaye, ghafla anaanguka sakafuni na kupoteza fahamu.
Kijana huyo mwenye umri wa wastani aliyekuwa amevalia fulana nyeusi na kaptula nyekundu aliingia kwenye gym kwa vishasha huku akionesha utayarifu na ujasiri wake kunyanya vyuma.
Ghafla alijijazia uzani wa vyuma katika pande zote mbili za chuma refu kisha kuanza kujitutumua kunyanyua uzani huo.
Hata hivyo, baadhi ya kuinua kutoka sakafuni na kufikisha katika eneo la kiuno chake, uzani ule ulionekana kumlemea na kumlazimu kuuachia na kuanguka Kwenda nyuma.
Mashahidi katika eneo la tukio walimkimbilia haraka kumsaidia, wakijaribu kumfufua, lakini kwa sasa haijulikani ikiwa alinusurika kwenye jaribu hilo.
Video hiyo, iliyoshirikiwa na mmoja wa watazamaji, ilisambaa kwa haraka mtandaoni, na kusababisha wimbi la hisia kutoka kwa watu wakielezea kutoamini na wasiwasi wao juu ya tukio hilo la kuogofya.
Video hiyo imevutia maoni mesto katika mtandao wa X ilikochapishwa. Itazame hapa:
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!