Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amejitokeza kumsaidia Irine Wambua - mwanamke aliyepofuka jicho baada ya kushambuliwa na fisi.
Akizungumza moja kwa moja katika Runinga ya Citizen Bwana Sonko alihiadi kumsaidia bi Wambua kwa matibabu ya Jicho lake ambapo jicho lake la upande wa kushoto lilipofuka pamoja na mkono wake kuliwa.
Wambua aliathirika kwa kulipoteza jicho lake la kushoto kutokana na uvamizi wa fisi waliotaka kumla, hio ni baada ya kutupwa nje ya Lori alimokuwa akisafiria.
Bi wambua alisimulia kwa kusema kuwa alikuwa amebebwa na lori ila wenye kumbeba waliazimia kumrusha nje na kumuwacha akiwa hoi.
Bi wambua alisema kuwa baada ya kutupwa nje aliweza kupatwa na fisi barabarani usiku huo ambapo aliweza kuliwa na fisi na hata kupoteza mkono wake wa kushoto vilevile.
''Nilijipata mahali ambapo kulikuwa na lori nyingi kando yake nilisikia mtu akiongea kikamba nikamuona kama mtu aliyekuwa kando nikamuona kama mtu ambaye angenisaidia'' .Bi wambua alielezea.
'' Nilikuwa mahali ambapo palikuwa panaitwa Mariakani baadaye tukiendelea na safari niliona wanaume wakitoa soda aina ya Mango waliniambai ninywe nikaataa'.Maskini wa Mungu Wambua alisimulia.
'' Tukiwa katika hali hiyo ya usafiri niliona maafisa wa polisi nilitamani kupiga nduru ila ikashindikana hapo ndipo niliona dereva akiwa amesimama na kuanza kutoa nguo mbele yangu suruali yake ikiwa imefika kwa mabgoti nikamuuliza mbona alikuwa anataka kunifanyia hivyo?''. Ireine aliendelea kuelezea masaibu yaliyomkumba.
Kufikia pale wanaume wale walimrusha nje hapo ndipo alipokutana na fisi aliyemuuma jicho pamoja na mkono wake na kumvuta hadi ndani ya fensi tayari kumuangamiza.
Hata hivyo aliweza kuokolewa na maafisa wa polisi waliokuwa wakipita na hatimaye kuona mwili wa binadamu ukiwa umevutwa hivyo kuweza kusaidiwa na kupelekwa kwenye kituo cha afya kupokea matibabu.
Kutokana na kisa cha Irine hapo ndipo Bwana Sonko aliposikia stori yake na kuguswa na simulizi yake hatimaya alipiga simu moja kwa moja situdioni na kuahidi kujitolea kumsaidia Bi Irine ili aweze kujinasua kutoka kwa masaibu yanayomkumba.
''Irine habari yako nimesikia stori yako kwa hakika inasikitisha sana hiyo kodi ya nyumba nitalipa kwa miezi mitatu halafu kuna madaktari wako hapa lion eye plant kutoka India hapa upper hili tutakusaidia usijali jipe moyo'' bwana Sonko alisema kwa matamshi yake mwenyewe.
Bi irine aliomba usaidizi wa kufanyiwa upasuji ili apate jicho kjingine jambao ambalio Bwana Sonko alijiokeza na kusema kuwa atamsidia kwa udi na ambari.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!