Sarah Mtalii, MD wa Bonfire Advwentures

MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya kusafirisha watalii ya Bonfire Adventures, Sarah Mtalii amekanusha madai kwamba amepata mpenzi mwingine baada ya kuondoka katika ndoa yake.

Akizungumza kwenye runinga ya KTN kwenye Art of Living na Naila Kenga, alisisitiza kwamba ni matarajio yake makubwa kupata penzi tena lakini kwa sasa bado hajapata mpenzi.

Hata hivyo, mkwasi huyo aliweka wazi kwamba yuko sokoni.

“Niko shopping lakini bado sijapata. Ninatarajia kuwa katika mapenzi,” alisema huku akikanusha uvumi kwamba kuna ushahidi unatembea mitandaoni akiwa na mtu.

Alisema kuwa ushahidi huo hauwezi kuwa wa kuaminika maana ulichapishwa na yeye mwenyewe.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Sarah Mtalii alikariri msimamo wake kwamba bado yuko single na akaweka bayana kwamba anatafuta si tu mpenzi lakini pia mfadhili kwa ajili ya kujenga zaidi wakfu wake unaolenga kukimu wanawake waliotoka katika ndoa za manyanyaso.

“Mimi bado niko single na kama ni kutafuta, ninatafuta wafadhili pekee kwa ajili ya wakfu wangu. Kwangu mimi nataka tu wafadhili kwa ajili ya wakfu wangu wa Virtuous Women.”

“Nimeanzisha kituo cha uokoaji kuwaokoa wanawake ambao huenda wamepitia udhalilishaji katika ndoa na mahusiano. Kwa sababu mara nyingi huwa wanakuja katika ofisi yangu na wanataka kulala kwenye sakafu,” alieleza sababu ya kuanzisha kituo hicho.

Mama huyo aliweka wazi kwamba anatafuta wafadhili wa kumpa msaada wa kifedha, magodoro na vitu vingine vya samani kama vitanda na viti.

“Nataka watu ambao wana uwezo wa kutoa chochote, inaweza kuwa sufuria, kiti au hata msaada wa kifedha hata kama uko na mia au mia mbili,” Mtalii aliomba.

Mjasiriamali huyo aliweka wazi mwishoni mwa mwaka jana kwamba ndoa yake ya miaka kadhaa ilikuwa imeyumba kumpelekea kutengana na mume wake ambaye pia ni mjasiriamali mwenza.

Katika mahojiano na Dr Ofweneke, Sarah Mtalii alifunguka kwamba kabla ya kufikia uamuzi wa kugura ndoa, alikuwa amehisi ndoa yenyewe ilivunjika takribani miaka miwili nyuma.

Alisema kwamba ni kawaida kwa wanawake kujitoa katika kitu kihisia kwanza na kisha kujitoa kimwili baada ya muda.