
DIOGO Dalot ameshiriki ufahamu kuhusu miezi ya mwanzo ya ukufunzi wa Ruben Amorim katika klabu ya Manchester United.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anasema uaminifu wa kikatili wa Amorim umepokelewa vyema na chumba cha kubadilishia nguo cha Red Devils.
Dalot alifichua kwamba katika siku za mwanzoni, Amorim alikuwa anajisahau na kuanza kuwazungumzia wachezaji Kireno bila kujali kama wanaelewa au la.
Beki huyo aliiambia talkSPORT: "Ilikuwa ya kuchekesha kwa sababu wakati mwingine alikuwa ameizoea hapo mwanzo, kuzungumza Kireno, kwamba angeanza kuzungumza Kireno kwa wachezaji wote. Na wachezaji walikuwa kama: 'Bosi, subiri kwanza, unazungumza [Kireno]. Na alikuwa kama: 'Oh, samahani!'
Hata hivyo, Dalot alimtetea Mreno mwenzake akisema kuwa ni hali ya kawaida kwa mtu kujisahau na kuzungumza kwa lugha aliyoizoea.
"Na tayari alianza na Kiingereza, lakini ni mabadiliko ya kawaida, nimekuwa huko. Nilipofika, ilikuwa sawa."
Dalot aliendelea: "Nadhani [kuzungumza Kiingereza] ni jambo ambalo kwa wazi alijaribu kuhakikisha mara tu alipofika, kuzoea haraka sana ili kila mtu asihisi [ametengwa].
"Ni wazi kwamba wakati mwingine ni rahisi kwake kuwasiliana kwa Kireno katika miezi michache ya kwanza. Lakini sasa nadhani ikawa kawaida kwake kuzungumza Kiingereza."
Amorim alikuwa chaguo la kwanza la United kuchukua nafasi ya Erik ten Hag wakati Mholanzi huyo alipofutwa kazi Oktoba.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 40 alikua mmoja wa makocha waliotafutwa sana Uropa wakati alipokuwa Sporting Lisbon, lakini amevumilia ubatizo wa moto huko Old Trafford huku Mashetani Wekundu wakiweka rekodi yao ya kumaliza ligi chini kabisa katika enzi ya Ligi Kuu.
Ingawa matokeo yamekuwa ya kupanda na kushuka, inatumainiwa Amorim ndiye atakayemaliza hali mbaya ya sasa ya United.
Hakika amewavutia wachezaji wake na majaribio yake ya kuzungumza Kiingereza tangu siku ya kwanza yalipokelewa vyema, kulingana na Dalot - hata kama mtani wake alirejea katika lugha yake ya asili.
Lakini Dalot anasema yeye na wachezaji wenzake wanathamini uaminifu wa meneja wao, akieleza:
"Nadhani ni moja ya pongezi nzuri zaidi unaweza kutoa juu yake, ni kwamba yeye ni mwaminifu. Nadhani unaweza kuona kwamba wakati anazungumza, hajaribu kutoa jibu sahihi. Anazungumza tu kutoka moyoni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!